Saturday, August 02, 2014

WAKALA FEKI NA PEPO YA UONGO: FUATILIA STORI YA KIJANA OSUMAR SEIDU YENYE FUNDISHO KWA VIJANA WENYE TAMAA YA KUCHEZA SOKA ULAYA

Na Baraka Mpenja, kwa hisani ya mtandao wa Goal.com OSUMAR SEIDU pengine alianza kuwaza kuwa anaelekea kutimiza ndoto zake za soka. Alipanda ndege mpaka nchini Urusi ambapo alifikiria kujiimarisha kama mchezaji wa soka wa kimataifa, na labda siku moja aiwakilishe timu yake ya Taifa ya Ghana.

Kumbe alikuwa amekosea sana. Alipewa uhakika wa kutimiza ndoto zake na jamaa mmoja aitwaye Jermaine Owusu-huyu alidaiwa kuwa na leseni ya uwakala wa wachezaji ya FIFA akifanya kazi na kampuni moja ya ‘Soccer Kick’.

Jamaa huyu alisemekana kuwa anaishi mji mkuu wa Urusi, kwahiyo Seidu alianza kuhisi ndoto zake za kutaka ufahari katika soka zinakaribia kutimia. “Kitu fulani kilienda ndivyo sivyo tangu mwanzo, ingawa sikuweza kujua ni nini kwa wakati ule.

Labda ilikuwa ni mipango iliyoshindikana,” anasema kijana huyo mwenye miaka 23. ‘Mipango’ anayoisema kijana huyu ni ile ya Owusu kuchukua dola za kimarekani elfu 3000 (sawa na milioni 4,800,000 za kitanzania) kwa ajili ya gharama za usafiri na malazi wakati wote ambao Seidu atakuwepo Urusi.

Seidu na mwenzake mwenye ndoto kama zake waliwasili Urusi wakiwa na matarajio makubwa ya kufanya majaribio. Owusu alitegemewa kuungana na wachezaji hawa wawili nchini Urusi muda mfupi ili kuona maendeleo yao kwenye klabu wanayotakiwa kufanya majaribio.

Cha kushangaza mambo yalikuwa tofauti na hatima yake ilikuwa ni nini? Seidu anasimullia kwa undani zaidi: “Baada ya kufika Moscow, tulipokelewa na Alhassan mmoja, Mghana aliyehamia katika mji huo. Kwa furaha alituchukua mpaka nyumbani kwake.

Mwenzetu mmoja, anayeitwa Kojo, alijiunga nasi baadaye. Cha kushangaza usiku, tuliambiwa tulipe dola mia 200 kwa ajili ya kodi ya nyumba na dola 100 kwa ajili ya kupata kibali cha kutembe huru kwenye mji na dola zingine 50 kwa ajili ya chakula. ‘Mbaya zaidi, Owusu hakuonekana mjini Moscow, licha ya kutuahidi kufika wiki moja tu baada ya sisi kuwasili.” Seidu na rafiki yake waligundua kuwa mwenyeji wao, Alhassan ambaye aliigiza kuwa mkarimu alikuwa muhuni na alishawahi kukaa jela nchini Urusi kwa miaka sita kutokana na kumiliki dawa za kulevya kinyume na sheria.

Alishikiliwa ndani ya ‘Obi manso’ (ardhi ya mtu mwingine). Seidu na rafiki yake wangehesabu nini? Wakala aliyeonekana kuwa msaada, aliwatupa na kuwatupa kabisa? Je wameingia katika mpango feki wa Owusu? Sasa wanafanyeje wakati wanaibiwa na watu ambao ni ndugu zao kabisa? Lakini bado walikuwa wanahitaji kupata nafasi ya kucheza soka na walikuwa na matumaini kuwa wakala wao atafika mjini Moscow.

“Baada ya karibia mwezi mmoja kumalizika bila kwenda popote, rafiki mmoja wa Kojo alitutembelea na kutupa mawasiliano ya watu wa michezo ambao wangekuwa msaada kwetu. “Bahati nzuri, muda si mrefu tulijitambulisha kwa makocha wengi wa akademi za Urusi,” Seidu anasimulia kwa tabasamu kidogo ingawa ni mazingira yanayoumiza.

Pale walifurahia sababu yao ya kusafiri maili 4,042 kati ya Ghana na Urusi ambayo ni kucheza mpira. Seidu anaendelea kusimulia, “ alitusafirisha sehemu nyingi kutafuta timu na alipata klabu ya kujiunga mjini Dagestan (jimbo matata huko Urusi ambapo timu kubwa yenye pesa ya Anzhi Makhachkala inapatikana), lakini ilishindikana kwasababu Viza yangu ilikuwa imeisha muda siku nyingi,” anajaribu kukumbuka, lakini anashindwa.

Seidu na mwenzake wakafika pointi ya kuamini kuwa sasa Owusu amewaingiza kichakani- mtu waliyemuamini sana na amewatupa kwenye ulimwengu wa huzuni na masikitiko makubwa.

Hawakuwa na sababu ya kuendelea kuishi kwenye Jimbo la Urusi wakiwa na nyaraka zilizoisha muda wake. Wawili hao wakagundua njia pekee itakayowanusuru ni kutafuta namna ya kurudi Ghana.

Lakini kichwa kikawagonga, watapata wapi tiketi za ndege? Kumbuka wametapeliwa fedha zao na Owusu. Waliumiza kichwa sana namna ya kupata tiketi za kurudi Ghana kutoka Urusi walipoamini wangetimiza ndoto zao. Pia walihitaji kutumia kiasi fulani cha fedha kulipia kibali cha kuishi nchini humo na fedha hizo zilichukuliwa na Owusu.

Mwenyeji wao Alhassan akabadilika kuwa mbogo na kutaka kulipwa dola 200 kwa siku saba zilizosalia, vinginevyo angewaacha mitaa ya Moscow ambapo ilikuwa rahisi kupoteza maisha. Seidu na mwenzake, Afful, waligoma kulipa fedha hizo na kutafuta njia mbadala ambapo waliamua kwenda ubalozi wa Ghana nchini Urusi ili kuomba msaada baada ya kushindwa kutimiza mahitaji ya mtu mbaya Alhassan ambaye hakuwa na huruma kwa ndugu zake na mhalifu mkubwa.
Aliwanyonya kila senti waliyokuwa nayo.

SAFARI YA KURUDI GHANA

Safari iliandaliwa na ubalozi, tarehe ya kuondoka ilikuwa septemba 9, 2010, ambapo Seidu anaikumbuka vizuri sana siku hiyo. Baadaye walitua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kotoka na walishangaa kukutana na Owusu asiyekuwa na aibu uwanjani hapo. Seidu anakumbuka vizuri tukio hilo. “Nilipandwa na hasira, sikujisumbua kusemezana naye ingawa alionesha nia ya kutaka kuzungumza nami, Mungu anajua zaidi,” Seidu anasema kwa uchungu.

Baada ya kushindwa kuzungumza na kutokea ugomvi, mazungumzo yaliahirishwa mpaka siku nyingine wakati ambapo hasira itakuwa imepungua. Seidu alienda ofisini kwa Owusu akihitaji kurudishiwa kiasi fulaini cha fedha alicholipa kwa ajili ya safari ya Urusi.

MATOKEO YAKE ILIKUWA NINI?

“Hali ilizidi kunichefua zaidi,” Seidu anasema. “Mara ya kwanza, aligoma kunipa ninachodai.I linichukua mwezi mzima na hatimaye kupata changu. Hata hivyo niliona kama ni fidia ya mateso niliyoyapa”. “Uzoefu alioupatakwa Owusu ulimfanya Seidu alipeleke suala hilo kwenye vyombo vya habari na jeshi la polisi, mpaka sasa jitihada zake zimegonga mwamba,”

FUNDISHO KWA VIJANA

Ujumbe unaopatikana hapa ni mwepesi sana, kiukweli: kama wewe ni kijana mdogo mwenye kipaji cha soka na unahitaji nafasi ya kucheza nje ya nchi, pita njia sahihi na usiwe na tamaa.

Usiongozwe na tamaa ya kupata mafanikio ya haraka. Fuata taratibu zote. Usitake kuruka kwa haraka, utaingizwa kichakani kama Seidu. Hata ukiona kwenye mitandao wanahitajika watu kama ilivyotokea kwa Seidu, kuwa mpole na usijiingize kichwa kichwa ili kukwepa athari aliyoipata kijana huyu wa Ghana. BONYEZA HAPA 

0 comments:

Post a Comment