Habari nyingine kubwa ya Tanzania ni mjadala wa kurudi au kutorudi bunge la katiba kwa vyama vya Upinzani ambavyo vilijiunga na kuwa Umoja wa katiba ya Wananchi (UKAWA) kwenye mchakato wa kuitafuta katiba mpya ya Tanzania.
Mbunge wa Nzega Hamis Kigwangalla (CCM) usiku wa August 1 2014 aliandika kwenye page yake ya twitter kwamba ‘nimepata taarifa kuwa sehemu ya kwanza ya mazungumzo ya kutafuta suluhu baina ya CCM na UKAWA imekwisha bila mafanikio ‘
Nalo gazeti la Tanzania Daima August 2 2014 limeandika >> UKAWA wakwepa mtego wa CCM, kitendawili kimeshindwa kuteguliwa baada ya mkutano wa mwisho wa kutafuta maridhiano kukwama ambapo kikao hicho kilichoitishwa na Msajili wa vyama vya siasa Francis Mutungi kilitawaliwa na mivutano mikali baina ya Wajumbe wa UKAWA na wale kutoka CCM.
Tanzania Daima wanaripoti kwamba kikao kilianza kwa mkwamo baada ya Wajumbe wa CCM kugoma kuanza kikao wakilenga UKAWA wasitumie umoja huo bali wajitambulishe kama vyama vyao lakini umoja huo uligoma
0 comments:
Post a Comment