Kocha mkuu wa Yanga sc, Marcio Maximo (kushoto) akimuelekeza jambo mshambuliaji wa klabu hiyo, Jerryson John Tegete (kulia)
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam YANGA SC inatarajia kuanika hadharani wachezaji watakaoitumikia klabu hiyo msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania bara na michuano ya kombe la shirikisho na wale watakaoachwa Agosti 17 mwaka huu.
Afisa habari wa Yanga sc, Baraka Kizuguto amekaririwa na baadhi ya vyombo vya habari jioni ya leo akisema kuwa zoezi la usajili linaendelea vizuri ambapo viongozi wa kamati ya usajili wanashirikiana kwa karibu zaidi na benchi la ufundi chini ya kocha mkuu, Mbrazil, Marcio Maximo. “Mwalimu anaendelea kufanyia kazi ripoti yake pamoja na kutaja wachezaji anaowahitaji. Siku itapofika ambayo ni Agosti 17, mwalimu ataweka kila kitu hadharani,” alisema Kizuguto.
Baada ya Maximo kuwasajili wachezaji wawili kutoka Brazil, kiungo mshambuliaji Andrey Coutinho na mshambuliaji Gleison Santos Santana ‘Jaja’, Yanga imefikisha wachezaji sita wa kigeni.
Kwa mujibu wa sheria inayotumika kwa wachezaji wa kigeni kwa sasa, kila klabu ya ligi kuu inatakiwa kuwa na wachezaji wa kigeni wasiozidi watano, hivyo Yanga inatakiwa kumuacha mmoja. Kumekuwa na mjadala mzito wa nani anaichwa hususani kwa Waganda wawili, Khamis Kiiza na Emmanuel Okwi, lakini Kizuguto alisema kila kitu ni Agosti 17 mwaka huu.
“Kuna Mbuyu Twite, Khamis Kiiza, Haruna Niyonzima na Emmanuel Okwi, wote hatima yao itajulikana Agosti 17, hapo itajulikana nani atabaki Yanga na nani ataondoka,” aliongoza Kizuguto.
Kama bado ujaungana nasi ili kila nikipata habari zikufikie kirahisi BONYEZA HAPA
0 comments:
Post a Comment