Watuhumiwa wa mauaji ya Mtawa Cresencia Kapuri (50) wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Parokia ya Makoka, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakihusishwa na wizi wa pesa katika Benki ya Barclays.
Watuhumiwa hao ni Hamisi Shabani (34), maarufu kwa jina la Carlos, mfanyabiashara, mkazi wa Magomeni, wilayani Kinondoni na Manase Genyeke (35), maarufu kwa jina la Mjeshi, dereva na mkazi wa Tabata wilayani Ilala.
Washtakiwa hao ni miongoni mwa watu wanane waliotiwa mbaroni wakituhumiwa kuwa majambazi, huku pia wakitajwa kuhusika na mauaji ya mtawa huyo.
Kapuri aliyekuwa Mhasibu wa Shule ya Sekondari ya Mwenyeheri Anwarite na Parokia ya Makoka, aliuawa kwa kupigwa risasi Juni 23, eneo la Riverside, Ubungo.
Hata hivyo, washtakiwa hao jana walipandishwa kizimbani wakikabiliwa na mashtaka ya wizi wa Pesa zaidi ya Sh479 milioni mali ya Benki ya Barclays, Tawi la Kinondoni. Washtakiwa hao waliunganishwa na washtakiwa wengine katika kesi hiyo ambao tayari walikwishasomewa mashtaka hayo.
Washtakiwa wa awali katika kesi hiyo ni pamoja na meneja wa tawi hilo, Alune Kasililika (28) na Meneja mwingine, Neema Batchu, Kakamie Julius (32), Iddy Khamis (32), Sezary Massawe (31), Boniphace Muumba (29) na Ruth Macha (30). Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni askari wawili wa Polisi, Koplo Bundala na S/Sajenti Iddy.
Wakili wa Serikali Mwanaisha Komba, awali aliiomba mahakama kufanya marekebisho katika hati ya mashtaka ya awali ili kuwaongeza washtakiwa hao wawili wapya na kisha kusomewa upya mashtaka yanayowakabili.
Hati ya mashtaka ya awali ilikuwa na washtakiwa tisa, lakini katika hati hiyo mpya baada ya kuwaongeza washtakiwa hao wawili, sasa ina washtakiwa 11. Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu Mkazi Nyigulile Mwaseba na itataj
Kama unataka upate habAri kwa haraka sana punde zinapotufikia BONYEZA HAPA
UKIONA TUKIO LOLOTE USISITE KUTUTUMIA PICHA WHATSAPP NO:06570352125 Festo saimon
0 comments:
Post a Comment