Friday, July 18, 2014

NDEGE YATUA BARABARANI UGANDA

Ndege hii ilikuwa inaelekea mjini Juba Sudan Kusini
Shughuli ziliathirika leo wilayani Mityana baada ya ndege kutua kwa dharura katika barabara ya magari ya Mityana.

Ndege hiyo N604AR, iliyokuwa imewabeba wanajeshi wa Marekani, ilitua katika eneo la Kiwawu umbali wa kilomita 22 kutoka wilaya ya Mityana.

Kwa mujibu wa mtandao wa Nation, kamishna wa wilaya Joel Walusimbi, alithibitisha tukio hilo akisema rubani wa ndege hiyo alilazimika kutua katikati ya barabara

Polisi walisema kuwa ndege hiyo ilikuwa inaelekea mjini Juba Sudan Kusini kutoka uwanja wa ndege wa Entebbe.

Kama bado ujaungana na mimi ili kila nikipata habari zikufikie kirahisi bonyeza link apo chini
>›>>>>>>> BONYEZA HAPA >>>>>


UKIONA TUKIO LOLOTE USISITE KUTUTUMIA PICHA WHATSAPP NO:06570352125 Festo saimon

0 comments:

Post a Comment