Unapozungumzia warembo wazuri ndani ya jiji la Dar es Salaam ni wazi kwamba huwezi kuacha kulitaja jina la Agness Gerald maarufu kama Masogange.
Jina lake limekuwa kubwa sana kutokana na mrembo huyu kujishughulisha na upambaji wa video za wasanii mbalimbali wa bongo fleva.
Historia ya Masogange: Kumbukumbu zinaonesha kuwa Masogange alizaliwa April 23 1988 kwenye hospitali ya mkoa wa Mbeya. Alisoma katika shule ya msingi na sekondari ya Sangu kabla ya kuendelea na Advanced Level na baadaye akaja Dar katika harakati za kutafuta maisha. Aliingia katika kazi ya kuuza sura kupitia video za wanamuziki mbalimbali kutokana na umbo lake kuonekana kuwa limekaa kibiashara zaidi.
Inaelezwa kuwa Masogange ametokea katika familia ya wacha Mungu na kwamba wazazi wake hawakuafikiana naye katika kujishughulisha na kazi ya kuuza sura katika video za wasanii wa muziki wa kidunia.... Mwenyewe anadai kuwa anashughuli zake binafsi ambazo humwingizia pesa hapa mjini na kumudu shida e ambaye anaishi na baba yake.
Umaarufu na Skendo zake: Masogange alianza kuvuma baada ya video yake ya utupu kuvuja mtandaoni. Katika video hiyo, Masogange alionekana akikata mauno mbele ya mwanaume aliyejificha sura yake huku akiwa uchi wa mnyama
Baada ya mauno hayo, sauti za kimahaba za mwanamke anayefanya mapenzi, tena akiwa katika hisia kali zilisikika katika video hiyo... Jina lake lilizidi kuwa maarufu pale alipohusishwa na skendo ya usafirishaji wa dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine ambapo baadae mahakama moja nchini Afrika Kusini alikokuwa anashikiliwa ilikanusha tuhuma hizo na kusema kuwa dawa hizo hazikuwa za kulevya bali za matumizi ya kimaabara kwa ajili ya tiba za kibinadamu. Miongoni mwa video zilizolipaisha jina la Masogange ni video ya mwanamuziki toka pande za Morogoro, Belle 9 iliyokwenda kwa jina la Masogange.
Video nyingine zilizotengeneza CV ya Video Queen huyo ni ya mkali wa sauti Barnabas Elias alias Barnaba Boy ya Magubegube na ile ya msanii Tundaman iitwayo Msambinungwa.
Mafanikio yake: Mafanikio yake hayako wazi sana lakini baadhi ya watu wanasema anamshiko wa nguvu kutokana na dili anazopiga ndani na nje ya nchi. Wengine wanasema ukiachana na uzuri wa umbo lake,Msogange hana mtaji mwingine anaoutegemea kwani hata dili nyingi anazopata zinahusisha mwili wake.
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment