Friday, May 16, 2014

TFF YAFUTA USAJILI WA DOMAYO

Mambo yanazidi kuwa mambo kwenye usajili wa ligi kuu wakati Azam wanajihakikishia kumtumia kiungo mkabaji Frank Domayo kuicheza Azam katika msimu wa 2014/2015 tamko zito limetolewa na shirikisho la soka kuhusu uhamisho huo.

Tamko la Tff linasema kwamba mpaka sasa awatambui uamisho huo wa domayo kutoka  Yanga kwenda Azam ikiwa inamaana kwa TFF uamisho huo haupo.

Shirikisho limesema uamisho huo kutaMmbulika ama kutotambulika itajulikana pindi tume iliyoundwa na TFF itakapomaliza kazi yake kushughulikia  uamisho huo.

Ufafanuzi huo umetolewa na katibu wa TFF  Mwesigwa selestine ambaye anasema TFF haitambui uhamisho huo kwa kuwa ilikuwa inasubiri ripoti ya uchunguzi wa domayo aliyesajiliwa na Azam akiwa kambini kwenye timu ya taifa uko Tukuyu mkoani mbeya.

Mwesigwa alisema uchunguzi ulioagizwa na Rais wa TFF Jamal Malinzi ushakamilika na kilichobaki ni kupitiwa upya kama Azam walikuwa sahihi au awakuwa sahihi kumsajili kiungo mkabaji Frank Domayo akiwa ndani ya majukumu ya timu ya taifa.

Kwa sasa atuwezi kulizungumzia kwani tayari ripoti ishakamilika na kilichobaki ni kupitiwa upya na kutolewa maamuzi sahihi juu ya kilichotokea siku husika alisema "msigwa"


Posted by festo saimon

0 comments:

Post a Comment