Friday, May 16, 2014

Fahamu mfanyakazi aliyefichua picha ya mkanda wa jayz akishambuliwa na solange

Mfanyakazi aliyefichua kanda inayomwonesha mwanamuziki Jayz akishambuliwa na shemeji yake Solange amefutwa kazi.

Kamera ya lifti ilinasa vurumai kati ya jayz na solange ingawa haikujulikana kilichosababisha vita hivyo kwenye lifti.

Kanda hiyo ya video iliyotolewa kwenye tovuti ya udaku kuhusu watu maarufu TMZ ikimwonesha dada wa Beyonce akimpiga Jayz baada ya tamasha la met mjini Los Angeles iliyofanyika mwezi mei tarehe 5.

Baada ya ugomvi mkali baina yao mlinzi aliingilia kati hata hivyo kanda hiyo haikuwa na sauti.

Hoteli hiyo inayojulikana kama "The standard" ilisema kuwa ilistushwa sana na tukio la kufichuliwa kwa matukio ya lifti na ikimtaja mfanyakazi huyo aliyefichua tukio hilo.

Hoteli hiyo iliongeza kuwa ingetoa habari zingine zote za ziada kwa idara ya kupambana na wakiukaji wa sheria.

Wawakilishi wa Jayz,Beyonce na Solange awajasema lolote kuhusu tukio hilo.


Posted by festo saimon

0 comments:

Post a Comment