Kipa wa Simba Ivo Mapunda amewaonya wanachama wa Simba kutorudia makosa tena ya kuwachagua viongozi wanaojari maslahi yao.
Akizungumza hilo leo mchana Ivo amesema Simba haitokuwa na maendeleo kama viongozi hawatakuwa wanafuata majukumu yaliyowaleta.
Alisema timu yoyote ili iwe na maendeleo lazima viongozi watambue majukumu yao.
Sikukaa kufikiria matumizi ya fedha za ofisi alizokabidhiwa.
Hali hiyo ni muda wa wanachama kuangalia sera za wagombea maana bila hivyo timu haitakuwa na mashiko.
Katika kipindi cha miaka minne iliyopita timu imekuwa kwenye ugomvi wa mara kwa mara ivo ni vizuli kuangaliwa upya na wanachama na mashabiki alisema.
Alisema kuwa wanachama wasipokuwa makini utaendelea ugomvi wa mara kwa mara na ivyo kusababisha kuwa vunja moyo wachezaji.
Kikubwa ni wanachama kuachana na ushabiki wa kijinga usio na maana wala maendeleo katika timu.
Posted by festo saimon
Posted by festo saimon
0 comments:
Post a Comment