Wednesday, August 27, 2014

TAZAMA JINSI VIROBA VILIVYOMFANYA HUYU MWANADADA...VIPI UNAWEZA KUTOKANAYE AUTI DEMU KAMA HUYU?!!

 habari zingine  BOFYA HAPA 

"SYLVESTER STALLONE (RAMBO) AFARIKI BAADA YA AJALI MBAYA YA GARI" UVUMI WAENEA KWA HARAKA MIITANDAONI

Muigizaji wa the  "Expendables 3" Sylvester Stallone amekuwa mmoja wa mastaa wa Hollywood ambao wamekuwa ni waathirika wa kuzushiwa kifo. Tetesi zilizosambaa kama moto unaounguza pori/ msitu hasa hasa kupitia mitandao ya kijamii, zilianzia kupitia ukurasa feki wa facebook.

Habari hii ambayo inaonekana kusababisha panic kubwa kwa mashabiki wa muigizaji  "Rambo" imepelekea kutumwa kwa salamu za huzuni kutoka kwa mashabiki wake mbalimbali kupitia mtandao wa twitter.

Elinda Hagan @ElindaHagan
Follow

I just heard about Sylvester Stallone! Another favorite actor if mine, RIP

Ripoti hizo za
kifo cha Rambo zinadai kuwa alipata ajali mbaya ya gari iliyosababishwa
na  dereva wake aliekuwa amelewa na kutokuona gari kubwa lililokuwa
likija mbele yake.

Hii sio maara ya kwanza kwa muigizaji huyo kuuliwa na internet, mwanzoni uvumi mkubwa wa kifo chake ulioripotiwa na Global Associate News zilidai kuwa Rambo alifariki kwa ajali iliyotokana na snowboarding.

Sylvesta
Stallon (68) yuko hai na mwenye afya njema. Baada ya "Expendable 3"
atakuwa aki-shoot instalment ya 5 ya film yake "Rambo".

Ukiachana na Sylvester Stallon, wengine waliowahi kuzushiwa vifo ni pamoja na Justine Timberlake, Miley Cyrus na Charlie Hunnam

DUH!! NENO MOJA KWA HILI DENDA LA CHRIS BROWN NA DEMU WAKE MPYA KARRUECHE TRAN

HILI NDO CHEZAJI LA KIBRAZIL LINALOTARAJIWA KUINGIA BARCA HIVI KARIBUNI

KLABU ya Barcelona imekubali kumsajili beki wa kulia Douglas Pereira kutoka Sao Paulo kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 3.19, vigogo hao wa Katalumya wamethibitisha jana. Uhamisho unaweza kupanda kwa Pauni Milioni 1.2 zaidi kwa ajili ya beki huyo mwenye umri wa miaka 24 kulingana idadi ya mechi atakazocheza katika klabu yake mpya. Pereira atajiunga na klabu hiyo ya La Liga kwa mkataba wa miaka mitano iwapo atafaulu vipimo vya afya wiki hii nchini Hispania.

Hili ndo chezaji la wenger lililo ipiga shetani lekundu kipigo cha mbwa mwizi

Chezaji la Wenger: Mshambuliaji Benik Afobe anayecheza kwa mkopo MK Dons ya Daraja la Kwanza kutoka Arsenal, akishangilia bao la nne alilofunga jana dhidi ya Manchester United mchezo wa Kombe la Ligi. United ilichapwa 4-0, mchezaji huyo akifunga mabao mawili
Benik Afoba (kushoto) akifunga bao la tatu pembeni ya Keane wa United

New AUDIO | Stereo ft Victoria Kimani - Wako [Never Let You Down] | Download

TETESI ZA SOKA ZILIZOSHAMILI KWENYE MAGAZETI MBALIMBALI YA LEO JUMATANO ZIPO HAPA

Boss wa Manchester United Louis van Gaal anataka kumsajili kiungo wa Juventus Arturo Vidal, 27, kwa mkataba wa pauni milioni 34 kiasi ambacho kitafikisha pauni milioni 200 za kununua wachezaji Old Trafford katika kipindi cha miaka miwili (Independent), United huenda wakamtoa Javier Hernandez, 26, kwenda Juventus, katika mkataba wa Vidal (Daily Express), Manchester United pia wanatarajia kutaka kumsajili Daley Blind, 24 kutoka Ajax kwa pauni milioni 18 katika siku chache zijazo (Sun), Arsenal wanaonekana kuzidiwa kete na Roma, kumsajili beki wa kati Kostas Manolas, 23 kutoka Olympiakos (Goal), Manchester United na Arsenal wamepata matumaini ya kuendelea kumfuatilia beki wa Roma Mehdi Benatia, 27, baada ya klabu hiyo ya Italia kuvunja mazungumzo na Bayern Munich (Daily Star), Arsenal huenda wakamfuatilia Danny Welbeck, 23, kutoka Man United, au Loic Remy, 27, kutoka QPR kuziba pengo la Olivier Giroud ambaye huenda akakosa kucheza kwa miezi mitatu kutokana na jeraha la kiwiko cha mguu (Daily Telegraph), Southampton wameanza kumfuatilia beki wa Atletico Madrid Toby Alderweireld, 25, na kuwazidi Monaco (Times), Tottenham wapo tayari kutoa pauni milioni 8 kumchukua nahodha wa Sevilla Federico Fazio, 27 (London Evening Standard) Chelsea wanazungumza na Roma kumchukua Mattia Destro, 23 (Daily Mirror), QPR wanakaribia kumsajili beki wa Liverpool Jack Robinson, 20 kwa mkataba wa pauni milioni 1 (Daily Mirror), West Ham wamemuulizia beki wa kati wa Bayer Leverkusen Philipp Wollscheid, 25, (Daily Mail), Sunderland, QPR na West Brom wanamtaka kiungo wa Leicester Andy King, 25, (Sun), AC Milan bado wanataka kumchukua Fernando Torres kutoka Chelsea, wakala wake akipendekeza kumchukua kwa mkopo, ingawa mshahara wake mkubwa unaonekana kuwa kikwazo (Metro), Napoli wataanza kumfuatilia tena kiungo wa Tottenham, Sandro kwa mkopo (The Times), Sporting wamewaambia Arsenal kuwa watakubali kitita cha euro milioni 30 kumsajili William Carvalho, kama Arsenal watakubali kumtoa Serge Gnabry, Francis Coquelin au Yaya Sanogo kwa mkopo (The Times), Everton wanakaribia kukamilisha usajili wa Samuel Eto'o. Roberto Martinez alikuwa akimtaka Danny Welbeck wa Man United, lakini alikatishwa tamaa na bei ya Pauni milioni 15 (The Times) na boss wa Inter Milan, Walter Mazzarri amewaambia watu wake kuwa wako huru kujaribu kumsajili Ezequiel Lavezzi kutoka Paris St-Germain (Tuttosport). Zimesalia siku sita kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Share hizi na wapenda soka wote

BAADA YA DI MARIA, VAN GAAL HIKI NDO KITU ANACHOPASWA KUFANYA KUEPUSHA VIPIGO HIVI VYA MBWA MWIZI

NA BARAKA MBOLEMBOLE Ushabiki ni kitu cha kwanza katika mpira wa miguu. Shabiki ni mtu anayependa ‘ kupita kiasi’ kile anachokuwa anashabikia. Kama huna sehemu unayoshabia basi si rahisi kupata ‘ ladha halisi ya mpira waiguu’. Kupitia timu nayoishabikia naweza kuona makosa ya kiufundi, kufurahia ushindi, na vilevile kupata maumivu makali. Leo hii, maisha ya furaha ya mashabiki wa Manchester United yapo katika mashaka, ile furaha ya kushangilia ushindi kila mwisho wa wiki si ya kuaminika tena. Lakini ni hapo shabiki anaweza kuona mapungufu ya timu yake, na pengine akajiaminisha kuwa ‘ usajili zaidi hauepukiki’. Kila mtu anaona udhaifu wa United hivi sasa. Baada ya kipigo katika uwanja wa Old Trafford kutoka kwa Swansea City siku ya ufunguzi, United ilisafiri hadi Kaskazini Magharibi mwa England na kuambulia sare ya kufungana bao 1-1 na Sunderland katika uwanja wa Stadium of Right. United imefanikiwa kumsaini kiungo mshambulizi wa kimataifa wa Argentina, Angl Di Maria kutoka Real Madrid kwa ada ya rekodi England, pauni million 60. Di mAria amevunja rekodi ya usajili iliyowekwa na Fernando Torres Januari mwaka 2011 alipojiunga na Chelsea kwa ada ya pauni million 50 kutoka Liverpool. Kabla ya msimu wa ligi kuu England kuanza, United ilikuwa katika kipindi kizuri cha maandalizi nchini Marekani. Huko waliweza kupata ushindi dhidi ya timu za AS Roma, Inter Milan, Real Madrid, Liverpool, kabla ya kuishinda, Valencia siku chache kabla ya kuanza kwa msimu. Timu ilionekana bora chini ya kocha mpya, Luis Van Gaal. Wachezaji wa safu ya ulinzi, Criss Smalling, John Evance, na Phill Jones walionekana kuimarika na kucheza vizuri katika mfumo wa 3-5-2 ambao unawapa uhuru wa kushambulia na kukabia katikati ya uwanja walinzi wa pembeni. Van Gaal ametokea kuwaamini sana wachezaji hao wa Kiingereza, lakini baada ya kushuhudia safu yake ya ulinzi ikiruhusu mabao mawili katika uwanja wa nyumbani dhidi ya Swansea, Van Gaal aliharakisha usajili wa mlinzi wa kushoto wa Argentina, Marcos Rojo kutoka klabu ya Sporting Lisbon. Rojo ana uwezo wa kucheza nafasi ya ulinzi wa kati lakini wakati huu Luke Shaw akiwa katika majeraha, Van Gaal alimuhitaji, Rojo kucheza nafasi ya beki wa kushoto ambayo kiungo, Ashley Young alicheza katika mchezo wa kwanza. Smalling aliumia katika mchezo dhidi ya Sunderland, na walinzi wengine si wa kuaminiwa moja kwa moja kwa sababu, Jones na Evance wote ni wachezaji wa ‘ wasiwasi’ ni wachezaji wazuri lakini muda wowote wanaumia. Kuondoka kwa manahodha wote wanne kwa mpigo ni tatizo lakini tatizo zaidi ni kuwa wachezaji watatu walikuwa sehemu ya ulinzi. Patrice Evra, Rio Ferdinand na Nemanja Vidic hawa walikuwa msingi wa timu katika ngome. Van Gaal hatajuta kuondoka kwa wakongwe hao, lakini mashabiki wataendelea kuona mapengo yao katika ngome ya United kama hataingia sokoni kuongeza walau mlinzi mmoja wa kati. Safu hiyo imekosa kiongozi sahihi, majukumu ambayo yalikuwa yakifanywa na Rio, Evra na Vidic. Usajili wa Di Maria umekuja wakati mwafaka. United hushambulia na kumaliza mechi kupitia pembeni ya uwanja. Huo ndiyo utamaduni wa kiuchezaji katika timu hiyo na Sir Alex Ferguson alifanikiwa kwa sababu hiyo. Van Gaal atapata shinda katika mfumo aliokuja nao, lakini ujio wa Di Maria unaweza kumsaidia kwa sababu tayari ana uhakika wa kuwa na winga wa hatari ambaye anauwezo wa kukimbia na mpira ama bila mpira katika eneo la pembeni ya uwanja. United ina uhakika wa kufunga mabao, lakini safu ya ulinzi haina uwezo mkubwa wa kulinda lango lao. Van Gaal ametumia pauni millioni 60 kumsaini, Di Maria, pauni millioni 16 kwa Rojo, na pauni millioni 17 kwa Shaw, wote hao hawajatia mguu uwanjani hivyo kuna uwezekano mkubwa wakainyanyua timu hiyo kuanzia wikendi ijayo, ila usajili wa nyongeza katika ngome utasaidia kuziba nyufa za wachezaji wanaokumbwa na majeraha ya mara kwa mara. Usajili wa bei mbaya wote ulichemsha England, Juan Sebastian Veron, Robinho, Fernando Torres, ila sitaraji hivyo kwa Di Maria. 0714 08 43 08

PICHA HII YA WAIGIZAJI WA MOVIE HUKO NIGERIA ...INA TATIZOGANI?... ITAZAME KWA MAKINI!!!