Friday, August 22, 2014

JAJA AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO YANGA SC

MSHAMBULIAJI Mbrazil, Geilson Santana ‘Jaja’ amefunga bao lake la kwanza akiichezea mechi yake ya kwanza, timu yake mpya, Yanga SC ikiibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji Chipukizi Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba. Jaja alifunga bao hilo dakika ya sita kwa kichwa akimalizia kona ya Haruna Niyonzima na limedumu hadi filimbi ya mwisho- akijiwekea kumbukumbu ya mwanzo mzuri Jangwani. Kocha Mbrazil, Marcio Maximo alipanga vikosi tofauti kila kipindi- akianza na Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima, Geilson Santana ‘Jaja’, Hussein Javu na Andrey Coutinho. Kifaa kweli; Geilson Santana 'Jaja' kulia amefungua akaunti ya mabao Jangwani leo Yanga SC ikiilaza 1-0 Chipukizi ya Pemba Kipindi cha pili 11 hao wote waliwapisha Juma Kaseja, Salum Telela, Edward Charles, Rajab Zahir, Said Juma, Omega Seme, Simon Msuva, Nizar Khlafan, Hamisi Kiiza, Jerry Tegete na Said Bahanuzi. Yanga imeweka kambi kisiwani Pemba kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambayo watafungua na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya mabingwa Azam FC Septemba 13, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Yanga SC waliomaliza katika nafasi ya pili msimu uliopita chini ya kocha Mholanzi, Hans va der Pluijm, watauanza msimu huu wa Ligi Kuu kwa mchezo na Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro Septemba 20, mwaka huu. Siku hiyo, mabingwa watetezi, Azam FC wataanza na Polisi Morogoro Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, wakat washindi wa tatu, Mbeya City wataanza na JKT Ruvu ya Pwani, Uwanja wa Sokoine, Mbeya Septemba 20 na washindi wa nne, Simba SC wataanza na Coastal Union ya Tanga Septemba 21, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mechi nyingine za ufunguzi za Ligi Kuu zitakuwa kati ya Stand United watakaoikaribisha Ndanda ya Mtwara Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Mgambo JKT wataikaribisha Kagera Sugar Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na Ruvu Shooting watakuwa wenyeji wa Prisons Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani. Na mdadisiblog/festosaimon

LUIS FIGO ATUA DARA TAYARI KUWASHUGHULISHA AKINA PAWASA JUMAMOSI TAIFA

Karembeu akiwa na Mkurugenzi wa kampuni ya TSN, Farough Baghozah kushoto, ambaye kampuni yake ndiyo inawaleta magwiji wa Real nchini
Nyota mwingine wa zamani wa Real Madrid, Christian Karembeu akiwa na Tuliy baada ya kuwasili nchini
Magwiji wa Tanzania wanaendelea na mazoezi Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo huo, kulia ni Stephen Nyenge, kushoto Boniface Pawasa
Mwanasoka Bora wa zamani wa Dunia, Luis Figo kushoto akiwa Said Tuliy kulia baada ya kuwasili mjini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kukichezea kikosi cha magwiji wa Real Madrid dhidi ya magwiji wa Tanzania Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Tuliy ni mmona wa Waratibu wea ziara ya magwiji hao nchini.

MOURINHO NAYE AMWAGIWA MAJI YA BARAFU, APIGA KELELE KAMA MTOTO

KOCHA WA CHELSEA, JOSE MOURINHO NAYE AMEINGIA KWENYE KALE KAMTINDO KAMA MAJI YA BARIDI BAADA YA KUMWAGIWA NA KUMWAGIWA NA KUPIGA KELELE UTAFIRIKI KAMA MTOTO. DIDIER DROGBA NDIYE ALIYEMCHAGUA KOCHA WAKE HUYO. KAMTINDO HAKO KAMEKUWA KAKIENDELEA KWA KASI KWA WACHEZAJI NA MAKOCHA KIBAO KUMWAGIWA MAJI BARIDI MAARUFU KAMA SOACKING

Thursday, August 21, 2014

JAMANI JAMANI..HIVI HAWA WANAFUNZI WALIKUA WANAONGEA NINI HADI KUFANYA HIVI?!!!