Wednesday, August 13, 2014

MAXIMO AANZA KUANGALIA ALICHONACHO KIIZA

Mshambuliaji Mganda, Hamisi Kiiza, ameanza rasmi mazoezi na klabu yake chini ya kocha mkuu wa timu hiyo, Mbrazil, Marcio Maximo ambaye anaangalia uwezo wa mchezaji huyo pamoja na wale wengine ambao wote walikuwa wakizitumikia timu zao za taifa.

Wachezaji ambao walikuwa timu za taifa za nje ni pamoja na Emmanuel Okwi, Haruna Niyonzima na Hamis Kiiza na wale wa Tanzania Kelvin Yondani, Mrisho Ngassa, Simon Msuva, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Oscar Joshua.

Straika huyo ameanza mazoezi rasmi klabuni hapo siku ya Jumatatu akitokea nchini kwao Uganda na kocha wa timu hiyo anataka kupima uwezo wa mchezaji huyo na kama ataridhishwa, ataendelea naye.

Uongozi wa Yanga umemtaka kocha Maximo kuangalia uwezo wa Waganda hao wawili kati ya Kiiza na Okwi ili wajue nani wa kumuacha kwa jinsi alivyowaona kwa kuwa idadi ya wachezaji wa kigeni imezidi na kufikia 6 hadi sasa huku ikiwa imebaki nafasi moja pekee ya mchezaji mmoja wa nje kuendelea kuitumikia klabu hiyo ambapo ni lazima mmoja tu afungashiwe virago.

Aidha, straika huyo alikuwa akifanya mazoezi kwa bidii huku mara kadhaa akionekana kuwa makini na alichokuwa akielekezwa na kocha ikiwa ni pamoja na kuzungumza naye mambo kadhaa katika mazoezi hayo.

VAN GAAL AMPA ROONEY UNAHODHA MAN UNITED

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa England, Wayne Rooney ametuliwa kuwa Nahodha wa kikosi cha Manchester United na kocha Louis van Gaal.

Mholanzi huyo amevutiwa shughuli ya mpachika mabao huyo wa England tangu aanze kazi Old Trafford na anaamini atakuwa chaguo sahihi kuwa kiongozi wa wachezaji wenzake katika timu. "Kwangu, wakati wote muhimu chaguo la Nahodha," amesema Van Gaal katika tovuti ya klabu hiyo.

EVERTON YASAJILI WINGA MGHANA WA CHELSEA

Anakwenda: Winga wa Chelsea na Ghana, Christian Atsu anatarajiwa kujiunga na Everton kwa mkopo wa muda mrefu

KLABU ya Everton imekubali kumsajili kwa mkopo wa muda mrefu kiungo wa Chelsea, Christian Atsu, kwa mujibu wa kocha Roberto Martinez.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana sasa anakwenda kupiga kazi Goodison Park kwa msimu wote wa 2014/2015, kitu ambacho sasa Martinez amethibitisha. Utaratibu wa mkopo umefikiwa baina ya timu hizo mbili, huku kigali cha kufanya kazi kikibaki kuwa kitu pekee kinachomchelewesha Atsu kuwa mchezaji wa tano kusajiliwa na Everton msimu huu.

 BONYEZA KUUNGANA NASI 

CHEKI CHELSEA DAY, WACHEZAJI WATAMBULISHWA, DROGBA NDANI

CHELSEA IKIWATAMBULISHA WACHEZAJI WAKE MMOJA MMOJA KABLA YA KUANZA KWA LIGI KUU ENGLAND.

BONYEZA HAPA KUSOMA   HABARI NYINGINE 

ANGALIA MADRID WALIVYOSHANGILIA KOMBE LAO LA SUPER CUP

NAHODHA CASILLAS AKIWA AMEINUA KOMBE LA SUPER CUP, HII NI BAADA YA KUICHAPA SEVILLA MABAO 2-0.

UNAIKUMBUKA ILE PICHA YA COUTINHO NA MWANAFUNZI WA LOYOLA HIKI NDO KINACHOENDELEA SASA

Uongozi wa Shule ya Sekondary ya Loyola ya Mabibo jijini Dar es Salaam, umewazuia waandishi wa habari kuhudhuria mazoezi ya Yanga.

Waandishi wamezuiwa a uongozi wa Loyola, kisa kikiwa ni kupiga picha ya yule binti aliyeomba sahihi ya mshambuliaji wa Yanga, Coutinho.

Binti huyo alimfuata Coutinho na kumuomba aweke saini kwenye mkono wake, naye kafanya hivyo, huku waandishi wakijinafasi kwa picha. Siku iliyofuata, picha za binti huyo zilijaa kwenye magazeti na mitandao.

Hali ambayo ikaonyesha kuukasirisha uongozi wa shule ambao ukazuia waandishi kuhdhuria mazoezi!

 ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO HUU NA TUNAOMBA SUPPORT YAKO KWA KUBONYA HAPA 

NI PATRICK PHIRI, KOCHA MPYA WA SIMBA SC

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam, Alikuja akaondoka bila kuaga, alirudi akaondolewa kwa sababu, sasa anarejea tena kwa mara ya tatu klabuni Simba SC kama mkufunzi mkuu wa idara ya ufundi.

Namzungumzia, kocha raia wa Zambia, Patrick Phiri ambaye anatua nchi leo akitokea kwao kujiunga na Simba kwa mara ya tatu katika kipindi cha miaka kumi’. Phiri ameandaliwa mkataba wa miaka miwili na atasaini mara baada ya kuafikiana kuhusu mambo binafsi.

Ni kocha mzuri ambaye wachezaji wengi hupenda kufanya naye kazi. Mahitaji ya lazima ya timu ni kupata ushindi kadri inavyotakiwa lakini hilo litawezekana kama mahusiano ya kijamaa yataboreshwa kati ya uongozi na kocha, kwa maana ya kumuachia majukumu yote ya ufundi mwalimu.

Mara ya kwanza, Phiri aliondoka na hakutaka kurejea kuifundisha timu hiyo alipotwaa ubingwa wa Tanzania Bara mwaka, 2004 na ilikuja kugundulika kuwa mwalimu huyo alichukizwa na kitendo cha baadhi ya viongozi kumuingilia katika majukumu yake ya upangaji wa timu na kumchagulia wachezaji wa kuwatumia.

Tabia hiyo bado ipo na inaendelea kuwahukumu makocha wengi klabuni Simba na hata, Mcroatia, Zdravko Logarusic ameondoka kwa sababu hizo.

Heshima ya mtu inategemea jitihada zake za ufanyaji wa kazi na kutimiza majukumu yake. Kupendana, kuheshimiana kindugu, viongozi wanatakiwa kuwaamini walimu ambao wamekuwa wakipewa kazi na kuwaacha wafanye kazi yao.

Simba wanatakiwa kuishi maisha ya kijamaa ambayo kila mtu, mchezaji, kiongozi na benchi la ufundi anatakiwa kujua wajibu wake wa uwepo klabuni. Anaijua Simba, amewahi kufanya kazi, na ana mafanikio makubwa, ni sababu tatu ambazo, Zacharia Hans Poppe amesema zimewashawishi kumrejesha kocha huyo bora wa Zambia, mwaka, 1999.

Ni ukweli ulio wazi kuwa rekodi ya Phiri ndani ya uwanja ni bora pengine kuliko walimu wote ambao wamewahi kufanya kazi klabuni hapo. Phiri alichukua nafasi ya Mkenya, James Siang’a mwaka, 2004 na aliweza kuifanya timu hiyo kuwa imara katika mashambulizi huku akiwatumia wachezaji wa nafasi ya kiungo katika safu ya mashambulizi. Shaaban Kisiga, Athumani Machuppa, Nico Nyagawa, Mussa Hassan Mgosi nyota hao walikuwa wachezaji wa kutegemewa katika ufungaji.

Phiri ambaye amewahi kucheza michuano ya AFCON, 1978 na 1982 pia amewahi kushiriki michuano hiyo kama kocha mkuu wa Zambia, mwaka, 2008 nchini Ghana ni mtu asiyeishiwa sababu za kwenda nyumbani mara kwa mara hali ambayo imekuwa ikiathiri utendaji wa timu ndani ya uwanja.

Mara ya mwisho alipoondoka klabuni, Simba alichukizwa na kitendo cha kuingiliwa katika majukumu yake na hivyo kuamua kutoongeza mkataba baada ya kufanya kazi kwa miaka miwili mfululizo na kuwa kocha aliyekaa kwa muda mwingi klabuni hapo katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.

Trott Moloto alidumu kwa mwezi mmoja baada ya kuchukua nafasi ya Phiri mapema, 2005.

 UNAPENDA MICHEZO BHAAS BONYA APA UJIUNGE NASI 

RONALDO APIGA ZOTE MBILI REAL MADRID IKIUA 2-0 NA KUTWAA NDOO KUBWA KULIKO ZOTE ZA UEFA

Wafalme wa Ulaya; Wachezaji wa Real Madrid wakifurahia na taji lao la Super Cup ya UEFA leo
Magalactico wapya: Kikosi kipya cha kwanza cha Real Madrid kilichotwaa Super Cup leo
Mambo safi kabisa: Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia Real Madrid Uwanja wa Cardiff City

MABAO mawili ya Cristiano Ronaldo, moja kila kipindi yametosha kuipa Real Madrid ushindi wa 2-0 dhidi ya Sevilla, zote za Hispania Uwanja wa Cardiff City mjini Cardiff na kutwaa Super Cup ya UEFA. Sifa zimuendee nyota wa Wales, Gareth Bale aling'ara akicheza kwenye ardhi ya nyumbani na kutoa mchango mkubwa katika ushimdi huo.

Ronaldo alifunga bao la kwanza dakika ya 30 na la pili dakika ya 49. Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Casillas, Carvajal, Pepe, Sergio Ramos, Fabio Coentrao, Kroos, Rodriguez, Modric, Bale, Benzema, Ronaldo. Sevilla: Beto, Coke, Pareja, Fazio, Fernando Navarro, Alex Vidal, Krychowiak, Carrico, Vitolo, Suarez, Bacca.

 KAMA WEWE UNAPENDA USIPITWE NA HABARI MBALIMBALI ZA KIMICHEZO BONYA HAPA 

Credit binzubery

VAN GAAL AENDELEZA MARAHA MAN UNITED, YAICHAPA 2-1 VALENCIA

Marouane Fellaini akiifungia Manchester United bao la ushindi dhidi ya Valencia
Shujaa wa leo: Fellaini (wa tatu kulia) akipongezwa na wenzake baada ya kuifungia Manchester United bao la ushindi

KOCHA Louis van Gaal ameendelea kuwapa raja mashabiki wa Old Trafford baada ya Manchester United leo kuifunga Valencia mabao 2-1 katika mchezo wa kirafiki.

Sifa zimuendee Marouane Fellaini aliyefunga bao la ushindi dakika ya 90 na ushei katika mchezo ambao, Wayne Rooney alikosa penalti kipindi cha kwanza iliyookolewa na Diego Alves.

United ilitangulia kupata bao kupitia kwa Darren Fletcher dakika ya 49 kabla ya Rodrigo kuisawazishia Valencia dakika ya 71. Kikosi cha Manchester United: De Gea; Jones, Smalling, Blackett; Young, Fletcher, Herrera, James; Mata; Rooney, Hernandez Valencia: Alves; Barragan, Vezo, Otamendi, Gaya; Parejo, J. Fuego, Andre Gomes; Feghouli, Alcacer, Rodrigo

 KAMA WEWE N MWANAMICHEZO NA UNAPENDA USIPITWE NA HABARI MBALIMBALI BONYA HAPA 

DIEGO COSTA AANZA MAMBO CHELSEA...APIGA ZOTE MBILI THE BLUES IKIICHAPA REAL 2-0

Onyo mapema: Diego Costa akisherehekea baada ya kuifungia Chelsea bao la kwanza Uwanja wa Stamford Bridge

MABAO ya mawili ya mapema kipindi cha kwanza ya Diego Costa yameipa Chelsea ushindi wa 2-0 dhidi ya Real Sociedad ya Hispania katika mchezo wa kirafiki kujiandaa na msimu.

Akicheza kwa mara ya kwanza kwenye Uwanja wa Stamford Bridge tangu aiongoze timu yake ya zamani, Atletico Madrid kuifunga timu ya Jose Mourinho katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Costa alihitaji dakika nane tu kuiteketeza Real Sociedad.

Alifunga dakika ya kwanza na saba na sasa anafikisha jumla ya mabao manne aliyoifungia Chelsea tangu ajiunge nato akitokea Atletico mwezi uliopita.

Kikosi cha Chelsea kilikuwa; Courtois, Ivanovic/Zouma dk82, Cahill/Azpilicueta dk45, Terry/Christiansen dk86, Ake/Luis dk45,Ramires/Oscar dk45, Matic/Van Ginkel dk82, Fabregas/Mikel dk71, Schurrle/Willian dk45, Costa/Torres dk60 na Hazard/Salah dk82. Real Sociedad: Zubikarai, Zaldua/C. Martínez dk59, Ansotegi/Mikel dk11, Inigo Martinez, De la Bella/Yuri dk72, Markel/Elustondo dk59, R.Pardo/A.Oyarzun dk72, Granero/Chory dk65, X.Prieto/Hervías dk72, Canales/ Hernandez dk72 na Agirretxe/Estrada dk65

 KAMA BADO UJAJIUNGA NASI BONYEZA HAPA ILI KILA TUKIPATA HABARI ZA KIMICHEZO ZIKUFIKIE KIRAHISI