Kutofanyika kwa show ya kimataifa iliyokuwa
ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi wa
Diamond jijini Stuttgurt, Ujerumani na
kusababisha uharibifu mkubwa, kulichukuliwa
na watu wengi kama ajali kazini. Sababu za
Diamond kuchelewa kupanda stejini
kulikotokana na kudai alipwe fedha yake
iliyokuwa imesalia kwa promota, ilikuwa ya
msingi kabisa. Na pia kampuni yenyewe
iliyoandaa show hiyo ilieleza kwa urefu
kilichosababisha na pia kuahidi show ya bure
kwa mashabiki wa Diamond.
Hilo lilipita na kila upande ukaganga yajayo.
Ijumaa hii Diamond alikuwa afanye show
nyingine jijini London, Uingereza. Bahati
mbaya show hiyo ambayo yeye mwenyewe
kama kawaida yake aliipigia promo sana,
haikufanyika. Kama ilivyokuwa ya Ujerumani,
mashabiki walimsubiri staa huyo kwa masaa
kibao wasimuone akitokea. Baada ya
kuonekana kunakucha bila dalili ya Diamond
kupanda jukwaani, wengi walianza kudai
warudishiwe fedha zao. Na kwa mujibu wa
mtu aliyekuwepo kwenye show hiyo, polisi
walisaidia kurejesha amani katika ukumbi huo,
lasivyo yangetokea kama ya Ujerumani.
Pia anadai kuwa promota wa show hiyo
alikamatwa.
“I was there brov it was maad trust me, even
police got involved with that shit, they had to
calm people down until seven in the morning,
people wanted their money back he I’ll pay
the price cause he got arrested,” ameandika.
Diamond amemtupia lawama promota huyo
ambaye si mara ya kwanza kufanya naye kazi
na kumuita tapeli.
“Tafadhari ndugu zangu wa UK!!!….kuweni
makini sana na promoter huyu (Victor – Dj
rule) mnaposikia kaandaa show, party au Hafla
yoyote…ni vyema kuziepuka na kutohudhuria
kabisa kwasababu ni tapeli…. si unajua aisifiae
mvua imemnyeshea… basi mie nimeloa
kabisa.”
Pamoja na kwamba Diamond hana makosa
katika hili, hawezi kukweka lawama kutoka
kwa mashabiki wake walio na kinyongo naye.
Shabiki hatotaka kujua makubaliano kati ya
msanii na promota. Anachojua yeye ni kuwa
show ilitangazwa kuwa itafanyika na yeye
akanunua tiketi kuja kushuhudia.
Si kazi yake kutaka kujua kama msanii
amelipwa fedha yake ama lah! Kama Diamond
alikuwa anamfahamu vyema DJ Rule kuwa si
mwaminifu, kwanini alikubali kufanya naye
show? Sijui makubaliano yao yalikuwa vipi,
lakini kwanini alikubali kulipwa fedha nusu
kabla ya kutumbuiza?
Ni yaleyale kama ya Ujerumani.
Wengi tunamchukulia Diamond kama mfano
wa msanii wa Tanzania aliyefanikiwa na
tunategemea kuwa makubaliano yake
yanapaswa kuwa kwamba promota anatakiwa
kumlipa ama fedha nusu, robo tatu au fedha
yake yote (kama anamuam ini) na kusaini
mkataba unaowafunga wote. Mara nyingi
mikataba husema fedha iliyosalia inatakiwa
imfikie msanii wiki moja ama siku chache
kabla ya show. Wengine hukubaliana fedha
hiyo alipwe msanii pindi anapowasili katika
mji huo ama anapofika hoteli.
Ninafamu kuwa Diamond na timu yake wako
smart mara nyingi lakini nash indwa kupata
jibu la kwanini makosa kama haya yanaendelea
kutokea tena katika show za kimataifa. Kuna
uwezekano mkubwa kama hajapoteza
mashabiki wengi, basi heshima waliyokuwa
nayo kwake imepungua.
Yeye na timu yake wanapaswa kuwa smart na
kusaini mikataba ya show isiyokuwa na ahadi
za kupeana fedha ili yobaki siku ya show.
Promota wanapaswa kujipanga na
wanapotafutwa na promota wenye longolongo
wasiwe na aibu kuwakatalia moja kwa moja
kutunza heshima yao.
Matukio kama haya yanaweza kuwa mabaya
kwa biashara pia kwakuwa baadhi ya promota
wa kimataifa hawapendi kufanya kazi na
wasanii wenye CV mbaya kat ika show zao
zilizopita.
Haya ni baadhi ya maoni ya watu mbalimbali
yanayofanana kiasi na ya kwangu.
kiswigogodfrey
Play back concert 2 times inabuma hiyo ni
kukosa management imara yenye kusimamia
mikataba yako. Umetoka bongo hadi UK bila
kujua mikataba yako. Hilo fans wako
haliwahusu wao ni burudani ndio haki yao
hayo mengine utajijua na promota wako. Na
kama jamaa amekupiga kama ulivyo post ni
vzr ukafuata taratibu za kisheria ndio zitoe
hukumu na ukishinda ndio umwanike kwenye
social network.Kama hujafanya hivyo tegemea
kesi ya madai kutoka kwa mshikaji ingawa
umeshapata hasara kwa kukosa umakini na
management yako, it’s over.
jamal_huwel
Men mara ya pili hii hebu badilisha system ya
mikataba yako. Pokea angalau 60% of the cash
kabla ya shoo. Watakuharibia mtaalamu wetu
tutakosa talent yako tena
Allykikasha
PLZ PLZ PLZ READ THIS….DIAMOND wewe
ushakuwa msaani wa kimataifa na watu nao
wanakufahamu,, jaribu kutafuta timu ya
uhakika mtu anayejua ishu ya marketing
professionally,, uwe na mwanasheri hata yule
wa kumlipa tu pale unapoingia mkataba,,
achana na waki BABU TALE wao umeneja wao
ni wa show za mikoani tuu,, then hana
creativity yoyote zaidi ya kuwanufa isha,,
jaribu now to change,, uwe na watu wenye
uwelewa na kitu unachokifanya,, Germany
imetokea ,, then BAB TALE anasema eti
imesaidia kukutangaza,, very stupid comment
then ISSUE SIO PROMOTERS ITAFIKIA SIKU
FANS NOW WATAONA KILA SHOWS ZAKO NI
ZA KITAPELI ,, PEOPLE THEY CHANGE.
carryandy
Acha kuwatangazia mashabiki wako show
kabla hujalipwa hela kamili, vinginevyo
unajiharibia biashara 2nd time hii, hujajifunza
tuu? Na sijui kama unakuwa na makubaliano
ya maandishi kabla hujajiingiza kuwambia fans
wako utkuwa somewhere. , jipange utaja pata
matatizo makubwa nchi za watu hizo oh!
rayna_rayna_
Mmmhh um not sure kama anaweza
kukufanyia ivyo maybe umeenda bila contract
ndo mana imetkea yote..next tym jipange na
team yko najua jamaa ni mtu mkubwa and
also unaweza kwenda mshitaki ubalozini kwa
kukupotezea mda na kukupotezea issue maybe
it will help
callyrissanen
Pia kuwa makini chibu. Hao police wa nchi za
wenzetu wakifanya mawasiliano unaweza hata
huko germany ushindwe kufanya show. Tafuta
mwanasheria wa hiyo mikataba yako. Na uwe
unamaliziwa kulipwa pesa za show unapofika
tuu kwenye nchi husika, msisubiri hadi muda
wa onyesho ndio muanze kudaiana. Inakuwa
rahisi kutoa tamko kwa mashabiki mapema
kama hutohudhuria mapema iwezekanavyo ili
wasisumbuke
irymamur_de_star
Inaonekana management yako haipo makini
kabisa kwan inatokea nn?? hadi mtu
anakutapeli cc mashabiki zako tunaumia xana
kuckia ivyo na maswal mengi juu ya hilo kwan
thamani yako ya show za nje inapungua xaxa
kuwa makini na hao bakoharam sio watu
wazuri kwako na huyu jamaa xaxa mi si oni
kazi yake @babutale mi nakupa pole xana
kwailo!!!! ila hujafafanua vzur juu ya hilo tujue
ilikuaje yani tujue mwanzo mwisho kwa
maelezo kwan tunahaki kama mashabiki zako
pendwa!!!! |
0 comments:
Post a Comment