| Ligi ya mabingwa wa ulaya imeendelea tena
leo kwa michezo kadhaa kupigwa katika
viwanja mbalimbali barani ulaya – kule Etihad
stadium Manchester waliikaribisha FC Bayern
Munich katika mchezo wa kundi E.
Mchezo huo uliowakutanisha mabingwa wa ligi
za Ujerumani na England ulikuwa mgumu na
mpaka kufikia dakika ya 90 bado matokeo
yalikuwa 0-0, sifa zimuendee Joe Hart wa City
kwa umahiri wa kuokoa michomo ya
washambuliaji wa Bayern.
Katika dakika 3 za mwisho za nyongeza
mchezaji wa zamani wa Man City – Jerome
Boateng akaiadhibu timu yake ya zamani kwa
kuifungia Bayern goli pekee na la ushindi
kwenye mchezo huo.
Boateng alifumu a shuti kali ambalo Hart
alijaribu kulifuata lakini likamshinda na kuipa
Bayern ushindi wa kwanza kwenye ambalo
linahusisha vilabu vya Spartak na As Roma.
Timu zilipangwa kama ifuatavyo:
Bayern Munich: Neuer 7, Rafinha 6.5 (Pizarro.
84), Boateng 7, Benatia 6.5 (Dante, 85),
Bernat 7.5, Lahm 6.5, Alonso 6.5, Alaba 7,
Muller 6.5 (Robben, 76, 5.5), Lewandowski
6.5, Gotze 7
Subs: Reina, Dante, Shaqiri, Pizarro, Rode,
Hojbjerg.
Scorer: Boateng, 89.
Manager: Pep Guardiola, 6.5
Man City: Hart 9, Sagna 6.5, Kompany 7,
Demichelis 6.5, Clichy 6, Nasri 5.5 (Milner,
58, 6) Fernandinho 6, Toure 5.5, Navas 6
(Kolarov, 87), Silva 7.5, Dzeko 6 (Aguero, 74,
5.5)
Subs: Caballero, Kolarov, Aguero, Lampard,
Mangala, Boyata.
Manager: Pellegrini, 6.5 |
0 comments:
Post a Comment