Monday, September 29, 2014

RONALDO ASEMA AHITAJI MAPUMZIKO

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Real Madrid,
Cristiano Ronaldo amesisitiza kuwa hahitaji
muda wa mapumziko katika hatua hizo za
mwanzo wa msimu.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno alipatwa na
tatizo la majeruhi mwishoni mwa msimu wa
2013-2014 na wakati wa michuano ya Kombe la
Dunia nchini Brazil.
Hata hivyo, Ronaldo amesisitiza kuwa kwasasa
yuko fiti na anataka kuendeleza makali yake
aliyokuwa nayo kwa mabingwa hao wa Ulaya
baada ya kufuinga mabao ya kutosha katika wiki
chache zilizopita.
Ronaldo alikaririwa akidai kuwa kwasasa wako
mwanzoni mwa msimu na anataka kucheza ili
kujijengea hali ya kujiamini na wakati utakapofika
wakati muafaka ukifika atapumzika ili aweze
kuwapa wenzake nafasi lakini huu sio wakati
muafaka.
Mpaka sasa Ronaldo ameshafunga mabao tisa
katika mechi nne za ligi alizocheza

0 comments:

Post a Comment