Kiungo wa kati wa timu ya manchester City
katika ligi ya soka ya Uiungereza Yaya Toure
amesema kuwa mabingwa watetezi wa ligi hiyo
ni sharti waonyeshe umahiri wao wakati
watakapochuana na Chelsea baadaye siku ya
jumapili.
Mancity ambao walishindwa kwa bao moja kwa
sufuri dhidi Mabingwa wa Ujerumani Bayern
Munich katika mechi za kuwania taji la kilabu
bora barani ulaya wamewachwa kwa pointi sita
na Chelsea ambao kwa sasa wanaongoza ligi
hiyo.
Wachezaji wa Liverpool
Wakati huohuo timu ya liverpool ilipoteza mechi
yake ya tatu kati ya tano ilizocheza katika ligi ya
Uingereza msimu huu baada ya West Ham
kuicharaza mabao matatu kwa moja katika
uwanja wa nyumbani wa Upton Park.
Mabao ya mapema ya West Ham yaliofungwa na
Winston Reid na Diafra Sakho yaliichanganya
Liverpool ambayo ilipata bao la kufuta machozi
kupitia Raheem Sterling.
Katika matokea ya mechi nyingine arsenal
iliirindima Aston Villa mabao matatu kwa bila
ugenini.
Southanmpton nayo ikaifunga Swansea bao moja
lililoingizwa kimywani na mchezaji wa timu ya
taifa ya kenya Victor Mugubi Wanyama huku QPR
ikitoka sare ya mabo mawili kwa mawili dhdi ya
Stoke City.








0 comments:
Post a Comment