Monday, September 15, 2014
 |
| Ukiongelea wenye mvuto kwenye sanaa hii
ya Bongo fleva,Linah anaweza kuwa juu ya
list,jina lake kamili ni Linah
Sanga,anakimbiza sana katika anga hizi za
bongo fleva, kwenye upande mzima wa
mvuto,wadau wanasema kuwa hawezi
kulinganishwa na msanii mwingine yeyote. |
 |
| Urembo wake ulijionyesha pamoja na kipaji
chake kizuri cha kuimba pale alipoamua
kushiriki mashindano ya Epic Bongo Star
Search,ndio Tanzania ilipoanza kuona
uwepo wake,Shaghala baghala ndiye video
yake iliyomuweka kwenye ramani ya bongo
fleva mwaka huu,nakufanikiwa kuzidi
kupata umaarufu,uzuri wake unaweza
kusema labda amechovya flani hivi. |
 |
| Ingawa aliweza kuonekana kwenye nyimbo
kadhaa za bongo fleva hapo mwanzo,
kupitia uzuri wake akiwa kama
model,mwisho wa siku akajaribu kuweka
vocal,zikakubalika,nakushirikishwa kwenye
nyimbo mbali mbali ikiwemo kaka
dada.Huyu si tu msanii wa bongo fleva,bali
ni Tv presenter na host katika events
mbalimbali,ukiachia mbali u-CEO of Kidoti
Lovig co. |
 |
| Sauti yake na uzuri wake kwa mara ya
kwanza kuonekana katika luninga,ni
kwenye video ya tabasamu ya Mr.Blue,ila
kutokana na uzuri wake,naamini asilimia
kubwa ya watu huishia kumuangalia Najma
tu,naamini hata asingekuwa na sauti nzuri
watu bado wangekuwa wanaangalia video
zake,mbali na uzuri huo yeye pia ni msanii
wa bongo fleva na kwa hivi sasa ana-hit na
track yake mpya ya Nimechoka
aliyomshirikisha Aslay. |
 |
| Maarufu kama Vee money yeye ni
recording artist, rapper, songwriter, na
mtangazaji wa vipindi vya television na
redio,mitandao mengi ya huko nchini
Kenya ili ripotiwa kumfananisha mrembo
huyu na mmoja wa wanamuziki wa destiny
child,Kelly Rowland.ndiye msanii anayetoka
poa kwenye kila aina ya vazi atakaloamua
atupie,unaweza kudhani kuwa ni model au
kwa nini hajawa model nakuchagua kuwa
muimbaji kwa jinsi alivyo tu |
 |
| Wengi humfananisha msanii huyu na
mkongwe wa muziki wa Bongo fleva
maarufu kama RayC,kuanzia macho,weupe
wake,sauti hadi jinsi anavyocheza unaweza
kusema kuwa ni mdogo wake Ray C,ila
uzuri wake ndio uitakaokuweka kwenye
luninga yako muda mrefu kumwangalia
video yake,badala yakusikiliza nyimbo.Ni
msanii aliyekuja kwa kasi kwenye Bongo
Fleva nakukubalika kirahisi na kubaki on
top hadi hii leo,ana-hit na nyimbo kama
Kizunguzungu,upepo,nashukuru umerudi
na nyingine nyingi. |
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment