Monday, September 22, 2014
 |
| Baada ya Man United kupokea kipigo kutoka
kwa Leicester City, miamba mingine ya ligi
kuu ya Uingereza Chelsea ilijitupa uwanjani
kucheza na Manchester City.
Mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa
Etihad umeisha kwa matokeo ya sare 1-1.
Dakika chache baada ya Pablo Zabaleta
kutolewa kwa kadi nyekundu Chelsea walipata
goli la kwanza kupitia mchezaji aliyetokea
benchi Andry Schurrle.
Akitokea benchi mchezaji wa zamani wa
Chelsea Frank Lampard aliunganisha krosi ya
James Milner na kuisawazishia Man City.
Mpaka mpira unamalizika Man City 1-1
Chelsea. |
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment