Nahodha wa Yanga, Nadir
Haroub ‘Cannavaro’ (wa
kwanza kulia, waliosimama
wima)
Na Baraka Mpenja, Dar es
salaam
KUMKUBALI mpinzani wako
pale anapokukaba koo katika
soka ni ushujaa mkubwa na
inaonesha kuwa wewe ni
mshindani wa kweli.
Kuna wachezaji, makocha,
viongozi na mashabiki wa soka
huwa hawataki kuzungumza
ukweli pale timu yao
inapofungwa au kushinda.
Siku zote mtu anapenda
kusifia chake, hata kama timu
yake ilicheza vibaya na kupata
magoli, basi atasifia mno.
Lakini itakuwa ngumu kusikia
akisema tulicheza vibaya
ingawa tumeshinda.
Kibongo-Bongo, Simba na
Yanga ndio habari ya mjini.
Mashabiki wa Yanga
wanajasikia furaha sana pale
wanapoona timu yao inapata
ushindi, hawajali sana namna
inavyocheza.
Jana Yanga walichuana na
Tanzania Prisons uwanja wa
Taifa na kushinda mabao 2-1.
Wakicheza pungufu kwa
dakika 52, Prisons walionesha
kandanda safi na kuitia presha
Yanga hususani kipindi cha
pili.
Yanga walijitahidi kucheza
vizuri sehemu ya kati na
mbele, lakini bado safu ya
ulinzi iliyoongozwa na Juma
Abdul, David Charles, Nadir
Haroub ‘Cannavaro, Kelvin
Yondani/Rajab Zahir,
iliendelea kuwa na ugonjwa wa
kujisahau.
Hata goli walilofungwa jana,
Cannavaro na Yondani
walizembea na kumuacha
Ibrahim Kasaka Hassan
akiruka juu na kupiga kichwa
huru kilichomshinda kipa
Deogratius Munish ‘Dida’.
Baada ya mechi mashabiki wa
Yanga walifurahia ushindi
ikizingatiwa walitoka kwenye
machungu ya kufungwa 2-0 na
Mtibwa Sugar uwanja wa
Jamhuri.
Baadhi ya mashabiki walikiri
wazi kabisa kwamba
wamepata pointi tatu, lakini
hali ilikuwa tete kwa upande
wa Yanga.
Ghafla wakati wakizungumza
hayo, akatokea nahodha wa
Yanga na beki kisiki maarufu
kama ‘Waziri wa Ulinzi’ wa
Yanga, Nadir Haroub
‘Cannavaro’.
Mzanzibar huyu alionesha wazi
furaha yake baada ya
kuwaongoza wachezaji
wenzake kupata ushindi mbele
ya timu iliyokuwa bora.
Cannavaro alisema: “Kwanza
ni matokeo mazuri. Prisons ni
timu nzuri na imeonesha
kwamba ina uwezo. Tumecheza
na kupata nafasi nyingi,
tumepata magoli na
tunashukuru kwa kupata
ushindi.”
Siku zote timu ikiwa pungufu
inacheza kwa bidii.
Wakipungua wanakuja mbele
zaidi, na kwasababu na sisi
tumeshinda tunalinda goli letu.
Walirejesha goli na tukaweza
kupata goli la pili, ila Prisons
ni timu nzuri na tunashukuru
kwamba tumepata ushindi na
kusogea mpaka nafasi ya
tano”.
“Bado tuna makosa madogo
madogo, nadhani kwenye
mazoezi tutajirekebisha.
Kwenye mechi dhidi ya JKT
Ruvu tutaongeza nguvu zaidi”.
Yanga watashuka dimbani tena
wikiendi ijayo (Oktoba 5
mwaka huu) kumenyana na
JKT Ruvu uwanja wa Taifa, Dar
e salaam.
0 comments:
Post a Comment