Wednesday, August 27, 2014
 |
Tunamshukuru
aliyeleta wazo
la kila kata
kuwa na shule
ya
sekondari.Shule
hizi kwa kiasi
zimesaidia
kufuta ujinga
kwa walio
wengi.Asilimia
kubwa ya
wanaomaliza
shule za msingi
wanapata
nafasi za
kuingia kidato
cha kwanza
tofauti na enzi
zile za
mwalimu na
mzee wa
ruksa.Heri
nusu shari
kuliko shari
kamili,Ingawa
shule hizi zina
walakini lakini
mchango wake
kwenye jamii
unaonekana.Tofauti
ya sasa na
zamani
inaonekana
kupitia shule
hizi.Wengi
hawajaelimika
ila
wamepunguza
shari kwa
kufuta
ujinga.Wengi
wao angalau
wanajua
kujieleza kwa
lugha ya
chakula,Pia
wengi wanajua
ukichanganya
hydrogen na
oxygen unapata
maji,ukichukua
sodium na
chlorine
unapata
chumvi na
ukitaka kupata
chumvi na maji
kwa pamoja ni
lazima
uchanganye
acid na base.
Hi ndio tunaita
chemistry
(kemia), kwa
ufupi kemia ni
masomo ya
atomi na
mkusanyo wa
atomi kuwa
molyekuli.Yaani
hizo atomi
ukizichanganya
utapata kitu
kizima
kinachoitwa
molyekuli,Hata
ndugu zangu
wajenzi
wanajua ili
upate zege
lazima
uchanganye
ingredients(vitu
vinavyounda
zege),Ili upate
zege lazima
uchanganye
maji,
kokoto,mchanga
na simenti kwa
viwango
maalumu.
Kwenye soka
tumekuwa
tukitumia
maneno kama
chemistry
(kemia) huku
wengi tukiwa
hatujui
chimbuko
lake.Mchezaji
ndio atomi
yenyewe na
timu ndio
molyekuli.Kitendo
cha
kuwaunganisha
wachezaji
katika timu
moja na
wachezaji hao
kuungana
katika mfumo
husika ndio
tunaita
chemistry
(kemia).Kocha
anaposhindwa
kupata
wachezaji
husika kwenye
mfumo husika
hapo ndipo
tunasema
kashindwa
kutengeneza
chemistry
kwenye timu.
Kocha wa
manchester
united Louis
van gaal kama
hakukimbia
somo la
chemistry basi
anataka
kutuonyesha
staili mpya ya
kupika chapati
kwa unga wa
muhogo.Van
gaal
amethubutu
kutengeneza
molyekuli ya
3-5-2 lakini
amekosa atomi
husika za
kutengeneza
chemistry.Watu
wa mpira
wanaelewa
kuwa nafasi ya
kiungo ndio
muhimu kuliko
nafasi nyingine
uwanjani.Kama
unavyojua
tafsiri ya
Kiswahili ya
neno kiungo
pia ndio hivyo
hivyo tafsiri
hiyo hutumika
katika
soka.Katika
soka viungo
ndio
huunganisha
mawasiliano
kati ya mabeki
na
washambuliaji.Timu
nzuri ni ile
yenye viungo
imara.Kwenye
kiungo ndiko
kwenye siri ya
mafanikio.Madrid,Bayern,City
na timu ya
taifa ya
Ujerumani
wanaijua siri
hiyo.Louis van
gaal anajaribu
kutuelewesha
Darren fletcher
ni mtu sahihi
kwenye safu
yake ya kiungo
lakini garry
monk na Gus
poyet
wametuonesha
uongo wa Louis
van gaal.Na
kama kocha
huyo
ataendelea
kuwa
king’ang’anizi
na stori yake
ya fletcher na
thom cleverely
basi ategemee
watu kuendelea
kupiga miyayo
na wakiichoka
stori yake
watamkimbiza
kama
hakukimbia
mwenyewe.
Manchester
united
imemsajili
Angel di maria
ambaye ni
mchezaji bora
wa real madrid
nyuma ya
Ronaldo na
Bale lakini
kiungo huyo si
dawa ya
gonjwa la
united.Hapa
van gaal
anajaribu
kusoma vizuri
stori ya dokta
wa muhimbili
aliyemfanyia
mgonjwa
upasuaji wa
kichwa baada
ya mguu.Kama
ni ukimwi di
maria ni
ARV.Ataongeza
kitu katika
timu ila
hatatibu
gonjwa la
united.Manchester
united inahitaji
kiungo mkabaji
mwenye roho
ngumu mithili
ya Nigel de
Jong.Kiungo
mwenye kariba
ya de jong
akisimama
vizuri na ander
Herrera hapo
ndipo utaona
makali ya
Wayne rooney
na van
persie.Kwa sasa
washambuliaji
hao
wanaonekana
si lolote si
chochote
kwasababu ya
atomi
walizounganishwa
nazo.
Ukiacha
kupwaya
kwenye nafasi
ya kiungo
Manchester
united
imepwaya pia
kwenye nafasi
ya mabeki
baada ya
kuondokewa na
wakongwe
Nemanja
vidic,Patrice
evra na
Ferdinand.Tegemeo
pekee kwenye
nafasi ya
mabeki wa kati
ni john evans
na phil
jones.Hapa
napo van gaal
inabidi
apatazame kwa
mapana na
marefu kama
anataka
kuirudisha
united ya sir
alex ferguson.
Manchester
haina tatizo la
washambuliaji
wala viungo
wasaidizi wa
washambuliaji
bali wana
tatizo la Kiungo
mkabaji na
mchezeshaji
sambamba na
mabeki wa
kati.Haihitaji
vyeti kugundua
matatizo
hayo.Macho
yangu
hayahitaji
kuvaa miwani
na hasilani
hayanidanganyi.
Nakubali sina
elimu ya
ukocha kama
van gaal ila
hata yeye
mwenyewe
alikili kuwa
timu yake
haina uwiano
mzuri(imekosa
balance),wala
siwezi ishi
ndani ya
kichwa cha van
gaal kujua nini
kapanga juu ya
hatima ya
Manchester
united ila
nnachoweza
kumwambia au
kumkumbusha
van gaal ni
kuwa kamwe
hawezi kupika
chapatti kwa
unga wa
muhogo..
Na
Alleen kaijage
0655106767
kaijagejr@gmail.com |
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment