 |
| Baada ya kumpokea kwa
mikono miwili, Simba
imeamua kumrudishia
Emmanuel Okwi jezi yake
namba 25.
Kabla ya kuondoka kwenda Etoile du Sahel
alipouzwa 'bure' na Simba chini ya Ismail
Aden Rage, Okwi alikuwa akitumia jezi hiyo.
Yanga pia walimpa jezi
hiyo, lakini leo Mwenyekiti
wa Kamati ya Usajili ya
Simba, Zacharia Hans Poppe
amethibitisha kuwa Simba
imempa Okwi namna 25.
Baada ya kupokea namba
hiyo, Okwi kesho anapaa
Zanzibar kuungana na
wenzake ambao wako kambini
kujiandaa na Ligi Kuu Bara. |
Habari zingine BOFYA HAPA
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment