Mkali wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka amesema kuwa katika maisha yake amejiwekea utaratibu wa kujiheshimu ndio maana anaheshimika na watu wa kila rika , tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma alipokuwa anakumbwa na skendo za mara kwa mara....
Akizungumza na mwandishi, Ndauka alisema kuwa akili aliyonayo sasa ni ya kikubwa na anaangalia malezi ya mwanaye ambaye naye atapenda akuwe akiwa na maadili mema ambayo yatamsaidia kujiepusha kuingia kwenye dimbwi la vijana wenye tabia mbaya....
"Najiheshimu ndo maana naheshimika, ukiwatafuta wasanii wa filamu nchini wenye heshima mimi huwezi kuniacha kwani najua silaha ya kuheshimika ni kujiepusha na wambeya ambao hutoa maneno huku na kupeleka kule, akili za kitoto nimeshaziacha na sasa ni mtu mzima na pia ninaitwa mama mtoto," alisema Rose Ndauka.
Rose alisema kitu kingine ambacho kinampa heshima katika jamii ni uamuzi wa kumpenda kila mtu na kutokuwa na visasi na mtu kwani wanadamu wote hawajakamilika hivyo ni vyema kusameheana kila wanapokoseana.
0 comments:
Post a Comment