Friday, August 29, 2014

KUHUSU OKWI, HANS POPPE AIBUKA AWAPIGA DONGO ZITO YANGA

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema walichokifanya Yanga, ndicho kinachowarudia. Hans Poppe amerusha dongo nilo Jangwani ikiwa ni kuonyesha kwamba Yanga walimsajili Okwi wakati Simba ikiwa inaidai Etoile du Sahel dola 300,000. “Lazima wajue unapomtendea mwenzako, kesho yake kinarudi kwako,” alisema Hans Poppe ambaye ndiye injini ya usajili ya Simba. Awali Hans Poppe alieleza kuwa Okwi ameomba kurudi Simba na wao wamempokea kwa mikono miwili. “Tumempokea baada kuipokea barua yake na kuijadili, kwa kuwa Yanga wamemuacha na hata FIfa inasisitiza wachezaji kupata nafasi ya kucheza ili kuepusha kuua vipaji vyao, tumeamua kuwa naye,” alisema Hans Poppe.

 ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG HII ILA TUNAOMBA UJIUNGE NASI KWA KUBOFYA HAPA 


Posted via Blogaway

0 comments:

Post a Comment