Sunday, August 03, 2014

KUELEKEA MSIMU MPYA: MAMBO KUMI WANAYOTAKIWA KUFANYA MANCHESTER UNITED………

Na Nicasius Coutinho Suso

1: Kiungo mkabaji.. Pengine Michael Carrick bado Ni kiungo mzuri Sana, na pengine Ni moja ya engine ambazo hazizungumzwi Sana, lakini Man U wanahitaji kiungo mwingine mpya wa ukabaji. Kiungo anayeweza kuilinda vyema ngome ya ulinzi, na kuunganisha vyema ulinzi na katikati mwa uwanja.

Haina ya kina Strootman, umri wa Carrick,pia ni Tatizo na yawezekana hasiepukane na majeraha Sana.

2: Uongozi katika ulinzi. Kaondoka Vidic, Ferdinand, Evra.. Hakuna kiongozi katika ulinzi, Evra pia hayupo, wakati mwingi tutawaona Smalling, Jones, Evans. Nadhani ni wakati wa kumpa uzoefu Evans katika hili. Kiongozi ni muhimu Sana.

3: Juan Mata….. Unataka Januzaj, Au Herrera, ama Valencia. Hapana Man U inamuhitaji Juan Mata aliyetimia. Akiwa safi huyu anaweza kukupa assist nyingi kuliko Coutinho na Silva na goli wastani wa Giroud. Huyu ndie anayetakiwa kuunganishwa na Rooney na Van Persie. Katika miguu yake kumetunzwa goli 25 kwa msimu, zake mwenyewe na assist, kama akitumiwa vyema.

4: Van Gaal na Biblia yake mashabiki na Imani zao. Pengine watu wanalipuuza hili, lakini hakuna mzigo mkubwa aliobeba Van Gaal kama mafanikio kombe la dunia. Aliwaaminisha mashabiki, ndio maana si haba wakampa imani Yao. Huyu inabidi aitumie biblia yake vyema, bahati mbaya hajasema lolote kubwa bado ya ni wapi amepanga kuwa kufikia mwisho wa msimu. Kikubwa ni mashabiki kupunguza imani kubwa kwa timu na kusubiri matokeo, maana kwa vyovyote vile presha ni kubwa kwa wachezaji na makocha.

Mashabiki wana imani kubwa kwa Van Gaal, Van Gaal naye Ana jukumu la kuwapatia uponyaji, biblia yake aikamate vyema.

5: Unahodha? Unamtaka Van Persie? Nadhani hapa inatakiwa akili kubwa, Rooney kashaanguka katika machaguo mbele ya Van Persie. Atacheza Tu nyuma yake, ni wazi hafurahii ili, ndio alipewa mshahara mkubwa lakini nadhani unahidha nao utatuliza kichwa chake. Vyumba vya kubadili nguo vitatulia hapa.

6: Mfumo… 343, 352, ndio inawezekana kabisa ukawa mkombozi wa Manchester msimu huu. Majeruhi ya Mara kwa Mara ya Rafael yamepunguza nguvu upande wa kulia, Shaw ni mzuri ILA bado Sio wa kuvaa viatu vya Evra kirahis, nimesikia hata Van Gaal kalalamikia fitness yake. Ndio kikosi cha huu mfumo anacho na wakati anaandaa kurudi katika mifumo asilia hii itamsaidia Sana.

7: Old Trafford… Achana na Camp Nou, huu ni uwanja ambao Fergie aliufanya usitamaniwe na mtu yoyote yule. Ulikuwa wa mateso na,kilio hasa. Khali ilikuwa tofauti msimu uliopita nadhani ni muda wa kurudisha morali ya uwanja. Ni wakati wa kuwafanya wachezaji watambue maana ya huu uwanja. Ubingwa siku zote fergie aliokota hapa, haikuwa rahisi mtu kutoka salama.

8: Kutokuwepo Champions League. Utashangaa kwanini nimeiweka hapa. Unajua kwanini Liverpool,waliwatezsa timu kubwa na mbio ndefu, hawakucheza Sana katikati ya wiki. Hapa ukizichanga karata vyema unafika kileleni. Van Gaal analijua hili, na anaweza kulitumia hili kuwapa morali wachezaji ya kupigana. Hii inaweza kuwaweka vyema maa,a hata miguu ya van Persie itakuwa salama kiasi, itacheza weekend Tu.

9: RVP & ROONEY………. Inawekana hasa wakawa ni moja ya washambuliaji bora Sana walio chini ya kiwango kwa sasa, wote Sio wale walioipa MU ubingwa msimu mmoja uliopita. Hata Uholanzi walihitaji miguu ya Van Persie baada ya kichwa cha mbizi wakaikosa, Rooney vile vile. Man U inawahitaji hasa kuanzia uongozi mpaka magoli. Hawa wanahitaji kurudi katika umahiri kama tunataka kuiona Man U juu tena.

10: Uwiano wa magoli ya kufunga na kufungwa. Kuna usemi wa kiingereza unasema Offense gives u a win but defense gives you championships. Yaani ufungaji unakupa ushindi wa mechi na uzuiaji unakupa ubingwa. Hili ndilo lilikuwa Tatizo la,Liverpool, walifunga Sana ila,pia wakafungwa Sana. Man U alifunga magoli chini ya 70 na akaruhusu 43. Wastani mbovu kabisa. Wakicheza hivi tena siwaoni kule juu, Lazima waliondoe hili. Ahsanteni

Je umeguswa na kazi zety na unapenda habari zikufikie kirahisi pande tuzipatapo BONYEZA HAPA 

0 comments:

Post a Comment