Sunday, July 06, 2014

Warioba ataja sifa za Rais 2015

Dar es Salaam. Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba ametoa dira ya urais katika Uchaguzi Mkuu ujao kwa kutaja sifa za rais anayefaa kuiongoza Tanzania.

Warioba alisema kwamba taifa la Tanzania linastahili kuongozwa na vijana wenye nguvu ya mwili na akili. “Mimi nafikiri tuangalie kati ya vijana tulionao, nani anatufaa kuiongoza nchi, tusirudi kuangalia wazee,” alisema Jaji Warioba.

Alitoa kauli hiyo alipokuwa akijibu maswali ya mwandishi wa habari hizi katika mahojiano maalumu yaliyofanyika wiki hii ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Kauli hiyo ya Jaji Warioba imekuja huku ukiwa umesalia takribani mwaka mmoja na miezi minne, kabla ya taifa kuingia kwenye kinyang’anyiro cha Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaoshirikisha vyama zaidi ya 23 vyenye usajili wa kudumu nchini.

Uchaguzi huo mkuu ambao ni wa tano wa vyama vingi nchini, unatarajiwa kulipatia taifa rais mpya, baada ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza muda wake wa utawala wa awamu ya nne. BONYEZA HAPA 


festo saimon 0657035125

0 comments:

Post a Comment