Wednesday, July 02, 2014

WALIO MUUWA MWANAFUNZI WA RUCO IRINGA KWA KUMCHOMA MOTO WAKAMATWA

Jeshi la Polisi mkoani iringa linawashikilia watu wanne ambao ni walinzi wa duka usalama waliokuwa wakilinda nyumba moja ya kulala wageni iliyopo Kihesa katika manispaa ya Iringa kwa tuhuma ya kumchoma moto mwanafunzi huyo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa Ramadhani Mungi alisema tukio hilo lilitokea Juni 24 majira ya saa tisa usiku baada ya wasamaria wema kutoa taarifa polisi kuwa kuna mtu anatembea akiwa anawaka moto.

Mungi alisema mara baada ya kupata taarifa hiyo Jeshi la Polisi lilifika katika eneo hilo na kumkuta Daniel Lema (25) akiwa ameanguka chini huku akiwa amefungwa mikono nyuma.

Kamanda huyo aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Mussa Nganga (28), Costa Mgayuka (38), Steven Kalole (24) na Samson Peter (24) wote wakazi wa Kihesa.

“Tulipopata taarifa tulifika eneo hilo kwa haraka na tukamkuta ameanguka chini tulimfungua ile mikono na kumchukuza vizuri tulimkuta akipumua kwa shida ndipo tukamkimbiza hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa kwa ajili ya kupata matibabu.”alisema Kamanda Mungi.

Alisema kuwa mwanafunzi huyo alikuwa baa moja inayoitwa Inbox bar inayomilikiwa na Katibu Mkuu wa zamani wa TFF, Frederick Mwakalebela akipata kinywaji huku akiangalia michuano ya mpira wa miguu (kombe la dunia) ambayo inaendelea nchini Brazili.“Mwanafunzi alikuwa anaangalia michuano hiyo ya mpira wa miguu kwenye baa hiyo na baada mpira huo kuisha aliondoka na kuelekea nyumbani kwako Kihesa kabla ya kufika nyumbani eneo hilo kuna nyumba ya kulala wageni iitwayo Glory lodge ambapo pembeni yake kuna grocery moja iitwayo Glory grocery akaingia hapo akifikiri ipo wazi ili aendeleze kinywaji,” alisema.Alisema wakati akigonga mlinzi wa nyumba ya kulala wageni Glory lodge ambae ni mmasai aitwaye Mussa Nganga alimuona na kumuita ndipo kijana akakimbia na baada ya kukimbialimfukuza na kuwaita wenzake watatu na kumfanyia kitendo kama hicho.
”alisema Mungi.

Baada ya kufikishwa Hospitali ya Rufaa ya Iringa, Lema aliendelea na matibabu yake mpaka alipokutwa na mauti juzi majira ya saa nane mchana. BONYEZA HAPA UONE 


by festo saimon phone 0657035125

0 comments:

Post a Comment