Sunday, July 06, 2014

SHAMBULIZI LAFANYIKA PWANI YA KENYA

Kuna Ripoti ya mashambulizi matatu katika maeneo ya pwani ya kenya karibu na mpaka wa kenya na Somali.

Maafisa wa polisi wilayani Lamu wanachunguza milio mikali ya risasi iliosikika katika kituo kimoja cha kibiashara karibu na mji wa Mpeketoni ambapo zaidi ya watu sitini waliuawa katika mashambulizi mawili mwezi uliopita.

Kusini mwa Mpeketoni, kituo kimoja cha polisi katika wilaya ya Tanaraiver kinadaiwa kushambuliwa huku baadhi ya nyumba zikichomwa. Kundi la wapiganaji wa kisomali Al-shabaab limekiri kutekeleza shambulizi hilo bila ya kutoa maelezo zaidi.

Mwandishi wa BBC nchini kenya amesema kuwa kuna polisi wengi katika maeneo ya pwani kufuatia shambulizi hilo la mwezi uliopita. BONYEZA HAPA 


festo saimon 0657035125

0 comments:

Post a Comment