Wednesday, July 02, 2014

Mwanaume abakwa baada ya kupanda lift ya mtu asiyemjua

Mwanaume mmoja amebakwa katika barabara ya daraja lenye shughuli nyingi mjini Newcastle baada ya kukubali kupanda lifti ya mtu asiyemjua.

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 24 aliingia kwenye gari hilo dogo mapema alfajiri ambapo alifanyiwa kitendo hicho cha ubakaji katika eneo lenye nyasi nyingi karibu na daraja la Redheugh, Newcastle.

Timu ya uchunguzi wa makosa ya ubakaji hivi sasa inaendesha msako wa mtu aliyetekeleza kitendo hicho na kuwataka mashuhuda kujitokeza hadharani. Afisa upelelezi kutoka mji wa Newcastle, Caroline Ord, amesema hili ni tukio baya zaidi kutendewa kwa kijana huyo ambapo sasa polisi wanafanya kazi bega kwa bega na mtu huyo kuhakikisha wanampata aliyetenda kosa hilo. BONYEZA HAPA 


by festo saimon phone 0657035125

0 comments:

Post a Comment