Friday, July 11, 2014

MABINTI WAKITANZANIA WANAVOTUMIKISHWA MADANGURONI CHINA PART 4

Munira Mathias, binti wa Kitanzania aliyekuwa akiishi China akitumikishwa kufanya ukahaba, alikimbilia Jimbo la Macau akitokea Guangzhou, baada ya muda wa viza yake kumalizika.

Kama tulivyoona katika gazeti hili jana, Macau nako hakukaa kwani alikimbilia kwa rafiki yake wa Kirusi, baada ya yeye na mwenzake, Candy kutishiwa na mabinti wenzao Watanzania kwa ‘kosa’ la kurekodi ujumbe wa kuomba msaada kisha kuurusha kupitia mtandao wa WhatsApp.

Munira (ambaye si jina lake halisi) aliondoka katika chumba alichokuwa amepanga na kuacha kila alichokuwa nacho, isipokuwa hati ya kusafiria, tiketi ya ndege na kadi ya chanjo ya kuzuia ugonjwa wa manjano.

Itakumbukwa kwamba wakati akikimbia kutoka Guangzhou, tayari Munira alikuwa amemeza vidonge kwa ajili ya kutoa mimba ambayo hata hivyo hakuwa anafahamu baba wa mtoto anayemtarajia, kwani siku alipobakwa na vijana wanne hawakutumia kinga yoyote.

Alitakiwa kumeza vidonge tisa alivyopewa kwa ajili ya kutoa mimba, huku moja ya masharti yake yakiwa ni kutokukutana na mwanaume katika kipindi hicho.

Hata hivyo hakuweza kutimiza masharti hayo kwa sababu alikuwa na shida ya pesa, hivyo alikuwa akimeza dawa huku akijiuza. Alikaa kwa rafiki yake wa Kirusi kwa siku nne na wakati huo vidonge alivyokunywa vilikuwa vimeanza kumzidi nguvu, hivyo alikuwa akilegea. “Nadhani nilikosea masharti, ile mimba haikutoka bali niliona uchafu wenye harufu ukinitoka na nikawaambia ukweli wale marafiki zangu kuwa nina mimba, nikapelekwa tena kwa daktari ambaye alinipa vidonge vingine ambavyo pia havikufanya kazi,” anasema. Anasema alilazimika kutoa mimba hiyo kwa daktari baada ya kufika Dar es Salaam ambako awali hakuwahi kuwaza kama angerejea, baada ya kuishi China kwa siku 91.

Wale marafiki zake wa Kirusi, waliamua kumvusha aelekee Hong Kong, kisha Tanzania, lakini, alikutana na vikwazo zaidi kwa sababu bado picha yake haikufanana na ile iliyopo kwenye hati ya kusafiria. “Waliniingiza kwenye chumba maalumu na kuanza kunikagua upya, wakaniambia nifumue nywele nilizosukia, ili wanihakiki,” anasema. Anasimulia kuwa alifanikiwa kupanda ndege kurudi nchini, akiwa ametimiza siku 91, kuanzia Januari 19 hadi Aprili 10 mwaka huu. “Ilikuwa ni tukio jingine ambalo sikuwahi kulitegemea maishani.

Sikudhani kama ningerudi tena nchini kwangu kwenye amani, sikuamini kwa kweli,” anasema. Asakwa na mwenyeji

Itaendelea ..kama bado ujAlike ukurasa wetu hii simulizi ya kwel isikupite BONYEZA HAPA 


UKIONA TUKIO LOLOTE USISITE KUTUTUMIA PICHA WHATSAPP NO:06570352125 Festo saimon

0 comments:

Post a Comment