Tunaendelea na simulizi ya binti wa Kitanzania ambaye alipelekwa China kwa ahadi ya kupewa kazi katika hoteli, lakini alipofika huko alianza kutumikishwa kwa biashara ya ukahaba.
Jana katika tovuti hii, binti huyo ambaye tulimpa jina bandia la Munira Mathias kutokana na sababu za kitaaluma, alieleza kwamba baada ya mateso mengi, viza yake ya kuishi China iliisha muda wake na alikuwa akiendela kuwapo katika mji wa Guangzhou kinyume cha sheria.
Wakati anasumbuka na masuala ya viza, alihisi kuwa na hali isiyokuwa ya kawaida, aliamua kununua kipimo cha ujauzito cha bei nafuu.
Kwa bahati mbaya aligundua kuwa alikuwa mjamzito ambao anahisi kuupata siku alipobakwa na Wanigeria wanne.
Munira anasema suala la yeye kushika ujauzito lilileta shida zaidi, kwani mwenyeji wake, Jacky alimweka kikao na kumsuta kwa hilo bila kujali kuwa alibakwa.
Mmoja wa wanawake hao ambao walikuwa wakifahamika kama ‘Boss Lady’ alimshauri kuwa atamtafutia mwanaume ambaye atamsaidia kutafuta daktari ili watoe mimba hiyo.
Alipofika kwa daktari, alipewa vidonge tisa ambavyo alitakiwa kulipia Yuan za China 600 (zaidi ya Sh100,000). Hakuwa na fedha hivyo alitakiwa kuendelea kujiuza licha ya kuwa hakuwa amepona ili apate fedha hizo.
“Baada ya muda nilipata fedha hizo na nilipewa vidonge, ambavyo hata hivyo haviharibu mimba kwa wakati huohuo bali taratibu sana,” anasema Munira.
Muda wa kuishi Guangzhou ulikuwa umekwisha na Munira hakuwa amepata viza, ilimbidi aondoke. Lakini mwenyeji wake alimwambia ni lazima atafute fedha ya kulipia viza usiku uleule. Akimaanisha akajiuze usiku huo na kupata fedha kwa ajili hiyo. Munira alilazimika kuingia mitaani usiku ule kusaka wateja kwa ajili ya kupata fedha za kwenda kuchukua viza hiyo Macau, jimbo jingine maarufu nchini China.
Mwenyeji wake alimwambia wakati anaondoka asubuhi siku inayofuata, asiondoke bila kumuaga. Aliporejea usiku wa manane alijiandaa kwa ajili ya safari ya asubuhi yake, licha ya kwamba hakuwa amepata fedha za kutosha.
Kulipopambazuka alikwenda kumuaga mwenyeji wake kama alivyoambiwa, lakini alishangazwa na kitendo cha mwenyeji huyo kumnyang’anya baadhi ya vitu kama nguo na viatu alivyomnunulia wakati alipofika nchini humo.
Itaendelea kesho usisahau kulike page yetu ili mwendelezo wa story hii isikupite BONYEZA HAPA
UKIONA TUKIO LOLOTE USISITE KUTUTUMIA PICHA WHATSAPP NO:06570352125 Festo saimon
0 comments:
Post a Comment