Sunday, July 27, 2014

KABURU AONEKANA NA SAADY KIPANGA WA MBEYA CITY.

Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange `Kaburu`

MAGUMASHI yameendelea kutawala katika usajili wa soka la Bongo ambapo viongozi wanazidi kujifanyia mambo kwa mahaba yao.

Taarifa za uhakika ambazo mtandao huu umezipata ni kwamba mshambuliaji hatari wa Mbeya City fc, Saady Kipanga  ameonekana  jijini Dar es salaam akifuatana  na makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange Kaburu.

Kamati ya usajili ya Simba chini ya mwenyekiti wake, Zacharia Hans Poppe haimhitaji Kipanga, badala yake inamtaka mshambuliaji wa Ruvu Shooting ya Pwani, Elias Maguri, lakini Kaburu analazimisha asajiliwe Kipanga.

Kwa sababu Kaburu ni makamu wa Rais anaweza kuwa na nguvu ya kumsajili Kipanga, lakini mwisho wa siku sio mahitaji ya timu na atakuwa amefanya hivyo kwa matakwa binafsi na mahaba yake.

Kaburu aliwahi kufanya jambo hili tena katika usajili wa Abdallah Juma na Paul Ngalema kutoka JKT Ruvu. Wachezaji hawa hawakuwepo katika mahitaji ya timu, lakini Kaburu akawasajili na wakaendelea kukaa benchi mpaka wakatimka zao na kujiunga na Mtibwa Sugar.

Kitendo kama hicho kinajirudia tena ambapo Kipanga anataka kuingia katika majanga hayo ya kurubuniwa na kwakuwa ana tamaa, atahitaji kupata hela za haraka, lakini nafasi ya kucheza itakuwa finyu.

Kama kweli anataka kusajiliwa kwa `staili` ya magumashi kiasi hicho, bila kujali uhitaji wa timu, ataishia kuharibu kipaji chake.

Mshambuliaji halali wa Mbeya City fc, Saady Kipanga. (P.T) pichani

0 comments:

Post a Comment