Monday, July 07, 2014

Dayna Nyange amtega tena Diamond Platinnum

Mwanamuziki anayefanya vizuri katika gemu Dayna Nyange amesambaza beat ya wimbo wake mpya ambao tayari ameshaurekodi kwa lengo la kuwapima wasanii wezi wa beats za wenzao kama wataufanyizia tena..

Hatua ya Dayna imekuja kutokana na malalamiko aliyowahi kuyatoa siku za nyuma ya kuibiwa beat ya wimbo wa Number One na msanii Diamond Plutnumz baada ya kumsikilizisha beat hiyo na kumtaka afanye naye collabo.

"Safari hii nimeacha akili yangu na hisia zangu zitawale katika kile ambacho nina kiamini kuwa ni sahihi kwangu hasa katika huu wimbo mpya, tayari nimeurekodi lakini nimewasambazia beat ili nione nani atakayethubutu kuiba kama ilivyokuwa mwaka jana," alisema Dayna ambaye hivi sasa inasemekana yupo kimapenzi na mshiriki wa big brother, Nando.

Licha ya Dayna kutomtaja Diamond moja kwa moja katika mtego wake huo lakini ukweli unabaki palepale kwamba aliwahi kumshutumu mwanamuziki huyo pamoja na prodyuza Sheddy Clever kwa wizi wa beat na kesi yao ilifika hadi Basata na Cosota BONYEZA HAPA 


UKIONA TUKIO LOLOTE USISITE KUTUTUMIA PICHA WHATSAPP NO:06570352125 Festo saimon

0 comments:

Post a Comment