KOCHA Mkuu wa Taifa Stars Mart Nooij amekificha kikosi chake Mbeya kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Msumbiji lakini katika maandalizi hayo amewatema wachezaji watatu akiwemo beki mpya wa Yanga Partick Ngonyani ‘Pato’ ambaye kuanzia juzi amejisalimisha kwa kocha wake Marcio Maximo ‘The Chosen One’.
Mbali na Pato, Noij amewatema kiungo mkabaji wa Simba Jonas Mkude na mshambuliaji wa Mbeya City ambaye kitaaluma ni mwalimu, Mwagane Yeya ambao wote wameshaondoka kambini mara moja wakiwaacha wenzao wakipewa kazi ya kuangusha mbuyu wa Msumbiji.
Pato alijisalimisha kwa Maximo juzi wakati akiwa na kikosi kizima katika mazoezi ya Gym ya Ciro kwenye Jengo la Quality Centre linalomilikiwa na mwenyekiti wao, Yusuf Manji lakini akaambiwa siku hiyo hawezi kuanza mazoezi licha ya kujiandaa vyema ambapo jana ndiyo alianza kazi rasmi.
Akimzungumzia beki huyo kinda aliyetokea Majimaji ya Songea kocha msadizi wa Yanga Leonardo Neiva alisema Pato ameonyesha uwezo wa kutosha katika mazoezi ya jana katika uwanja wa Shule ya Sekondari Loyola ambapo wataendelea kumsoma taratibu.
“Tumemuona Pato ni kijana mdogo ameonyesha kuelewa na kushika kila unachomuelekeza kwa haraka tunaamini atakuja kuwa vizuri kwa sasa ni mapema kusema lolote kuhusu kiwango chake zaidi nafikiri tuachie tuendelee kumjua taratibu,”alisema Neiva.
0 comments:
Post a Comment