Tayari mpaka sasa abiria zaidi ya 300 wamepoteza maisha kwenye ajali tatu za ndege zilizotokea ndani ya wiki moja kuanzia wiki iliyopita ambazo ni ndege ya Malaysia, nyingine huko Taiwan na nyingine iliyoanguka Mali.
Matukio ya ndege yanaendelea kukaa kwenye wino wa vichwa vya habari baada ya hili jingine la ndege ya Sunwing ambayo ililazimika kukatisha safari na kurudi ilikotoka baada ya maneno ya kijana wa miaka 25 raia wa Canada kuongea na muhudumu wa ndege na kusema anataka kuilipua Canada.
Ndege hiyo iliyoruka saaa moja asubuhi Ijumaa July 25 2014 ikiwa na abiria 181 kutokea Toronto Canada kuelekea Panama City ambapo kijana huyu aliongea na Muhudumu aliekua anapita na kumwambia jinsi sigara zilivyo bei ghali nchini Canada na kwamba anaichukia nchi hiyo.
Baada ya hapo kijana huyu aliongea kwa kujiamini na kwa sauti ya msisitizo na ishara za mikono kwamba anataka kuilipua Canada.
Muda mfupi baada ya hiyo kauli Muhudumu wa ndege alitoa taarifa na ndege hiyo ikaamrishwa kugeuza kurudi ilikotoka wakati huohuo pia ikiwa inasindikizwa na ndege mbili za kivita zilizopewa amri kuifatilia zikiwa zinafaya mazoezi. Baada ya kutua tu saa mbili na dakika 55 ikabidi Polisi waingie ndani wakiwa na silaha na kumchukua kijana huyu aitwae Ali Shahi na kuanza kumuhoji hapohapo uwanja wa ndege ambapo alitarajiwa kupelekwa Mahakamani saa tatu kamili asubuhi.
Hata hivyo baada ya taarifa kuenea, baba wa huyu mtoto amejitokeza na kusema mwanae amekua na matatizo ya akili toka akiwa na umri wa miaka 16 hivyo alichosema hakuwa anamaanisha.
0 comments:
Post a Comment