Uongozi wa klabu ya Yanga Africans unapenda kuwajulisha wanachama wa Yanga wapenzi na wadau wa soka kwa ujumla kuhusu taarifa za kuhama kwa wachezaji wake Frank domayo na Didier Kavumbagu kuwa zisiwakatishe tamaa kwani ni mapenzi ya wachezaji wenyewe kwani walishakubaliana na uongozi kuendelea kuitumikia yanga kabla ya wiki mbili kuonekana wakiwa na wanaramba ramba.
Kuhusu Frank Domayo kuripotiwa kujiunga na timu ya Azam fc pia yeye alikuwa katika makubaliano ya kuongeza mkataba.
Tarehe 12/7/2013 domayo alikubaliana uongozi wa yanga kilichobaki ilikuwa ni kuweka sahihi kwenye mkataba mpya. Lakini domayo alisema hawezi kusaini mpaka atakapokuja mjomba wake ambaye ndiye wakala wake ahadi iliendelea mpaka ivo ivo mpaka mwaka ukakatika. Sisi kama yanga juzi kuona Domayo akijiunga na wana rambaramba
Habari izi zimewashitua wapenzi na wanachama wa yanga lakini ukweli ni kwamba wachezaji wenyewe walishindwa kuwa wa kweli.
Aidha uongozi wa yanga fc unawaomba wanachama wake na wapenzi wa Yanga fc wasiwe na wasiwasi juu ya kuondoka kwa wachezaji hao kwani bado yanga ina wachezaji wenye vipaji.
Posted by festo saimon
0 comments:
Post a Comment