Pambano la kugombea mkanda wa UBO kati ya bondia Karama Nyilawila na Daudi Mbelwa usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Hotel ya friends corner Manzese. Lilivunjika raundi ya nane baada ya mabondia kushuka chini ya ulingo na kuanza kuzichapa kavukavu.
Mabondia hao walifika hatua hiyo baada ya kukamiana kupita kiasi hali iliyowapelekea kusahau sheria na kuzichapa kiadui.
Licha ya pambano hilo kuvunjika mwamuzi, Antoni Ruta alisema kuwa Nyilawila alikuwa anaongoza kwa point.
Posted by flavian kachira
0 comments:
Post a Comment