Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limepga marufuku ngoma za kitamaduni ambazo hufanyika nyakati za usiku. Kwenye maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam ikiwa ni muendelezo wa kukabiliana na vikundi vya kiharifu ambayo yamekuwa tishio kwa usalama wa Raia.
Kufuatia kuibuka kwa vikundi vya kiharifu kama Panya road,watoto wa mbwa,mbwa mwitu ambao wengi wanahusishwa na ngoma hizo na kufanya uporaji na upigaji wa watu.kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Sulemain Kova amesema ni marufuku ngoma yoyote ya asili kuchezeka wakati wa usiku.
Kamanda kova amesema kutokana na operesheni inayoendelea tayari wameshakamata wafuasi zaidi ya 100. Ambao watu wengi wamekuwa wakilalamika vitendo viovu vinavyofanyika usiku wakati wa ngoma hizo maarufu kama vigodoro pamoja na baikoko.
Posted by flavian kachira
Posted by flavian kachira
0 comments:
Post a Comment