Kocha wa mwadui fc na kocha wa zaman wa simba Jamhuri Kiwero Julio amejitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya makamu wa Raisi katika uchaguzi mkuu wa simba utakaofanyika Jun 29 mwaka huu.
Julio alichukua fomu jana huku uamuzi wake ukipokelewa kwa hisia kwa wapenzi wa soka hasa mashabiki wa Simba sport club .
Ambapo uchaguzi huo umeonekana kuungwa mkono na watu kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu.
Julio amekuwa mtu wa nne kwa nafasi ya umakamu wa Rais ambapo itakuwa ni ushindani wa aina yake baada ya majina kadhaa kusuguana vikali.
Jana saa kumi ili kuwa mwisho wa kuchukua fomu kwa nafasi mbalimbali.
Posted by festo saimon
0 comments:
Post a Comment