Saturday, May 17, 2014

GONJWA JIPYA LAZUKA BONGO

Majanga huku hali ya sintofahamu ikiendelea kuwakumba wakazi wengi wa jijini Dar es salaam kufuatia kuzuka kwa ugonjwa wa dengue gonjwa lingine lisilo na chanjo wala tiba limezuka  jombitz linakuwa la kwanza kukujulisha.

Gonjwa liitwaro  CHIKUNGANYA linasambazwa na virusi jamii ya Alphavirus ambao huingia mwilini mwa binadamu endapo mtu ataumwa na mbu aina ya Aldes agypti (wanaosambaza homa ya dengue).

Kwa kawaida mbu wanaobeba ugonjwa huo hung'ata wakati wa mchana na baada ya hapo virus hivyo huingia  kwenye mwili wa binadamu huchukua muda wa siku mbili hadi tatu kabla ya dalili za awali kuonekana

DALILI
Kwa mujibu wa ripoti za kitalamu iliyotolewa na jopo la madaktari wa shirika la afya dunian WHO dalili za ugonjwa huo zinafanana kiasi kikubwa na zile za homa ya Dengue ambazo ni homa kali,maumivu ya kichwa,viungo kuuma na kuvimba na kutokwa na vipele vinavowasha mwili mzima.
Dalili nyingine ni kutapika  kuhisi kizunguzungu na mwili kuishiwa nguvu.

Ripoti hiyo imeongoza kuwa japo kuwa ugonjwa huu usababisha vifo vya ghafla ukimpata mtu atayechelewa  kupata matibabu husababisha ulemavu wa kudumu kutokana na virusi vya ugonjwa huo kushambulia viungo (joint) vya miguu mikono na shingo.

MATIBABU.
mpaka sasa hakuna chanjo wala tiba ya ugonjwa huo isipokuwa kinachofanyika ni kutibu dalili alizonazo mgonjwa wataalam hao wakaenda mbele kueleza kuwa kwasababu ugonjwa huo hauna chanjo wala tiba ni vyema watu wakajikinga wasing'atwe na mbu huyo ambae kwa kawaida hung'ata wakati wa mchana.


Posted by festo saimon

0 comments:

Post a Comment