Tuesday, August 05, 2014

Monday, August 04, 2014

Video: Mwanamke atoa nguo na kubaki mtupu mbele ya sanamu ya hayati Nelson Mandela Afrika Kusini mchana kweupe!

Kisa cha mwanamke mmoja nchini Afrika Kusini aliyevua nguo zote na kubaki na suti yake ya kuzaliwa na kusimama mbele ya sanamu kubwa ya hayati Nelson Mandela, kimewaacha wapita njia na majirani waliokuwepo karibu na eneo hilo midomo wazi.

Kwa mujibu wa gazeti la Star, Jumatatu mchana ya wiki iliyopita mwanamke huyo ambaye hakufahamika alifika eneo la Sandton, Johannesburg ilipo sanamu hiyo akiwa amevaa vizuri. Ghafla akafanya kama ambavyo hufanya wakati wa kuoga, alitoa nguo zote na kusimama mbele ya sanamu hiyo na kuwapa watu onesho la bure huku wengine wakichukua picha na video exclusive za kupost katika mitandao ya kijamii.

Hata hivyo mwanamke huyo alipomaliza kufanya alichokuwa anakifanya (ambacho hakijulikani) alivaa nguo zake moja baada ya nyingine tena taratibu kama yuko chumbani kwake na kuondoka huku watu wakimshangaa.

Kama bado ujaungana na sisi ili kila tukipata habari zikufikie kirahisi  BONYEZA HAPA kujiunga nasi

New Music: Dogo D Ft King Silver – Wamenichokoza #3 download hapa

Sikiliza Muendelezo wa Msanii kutoka Rock City Mwanza Dogo D wangoma yake “Wamenichokoza 3″ akimshirikisha King Silver Producer J Monster Studio Megga Town Records
>>>>>> DOWNLOAD AU KUSIKILIZA HAPA \\<<<<<<<<<<<<

Kama bado ujaungana na mimi ili kila nikipata habari zikufikie kirahisi BONYEZA HAPA 

Bibi wa mjini Songea ajitengenezea jeneza ili akifa azikwe nalo

Mkazi mmoja wa Kijiji cha Lundusi Kata ya Peramiho wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma,Bibi Scholastica Mhagama amesema miaka mingi ameishi maisha dhiki na kunyanyaswa bila msaada kutoka kwa jamii anayoishi hali ambayo imemfanya amuombe Mungu amchukuwe ili azikwe kwenye jeneza alilojiandalia.

“Kila siku naomba Mwenyezi Mungu anichukue haraka ili nikapumzike kutokana na mateso ninayoyapata, lakini hofu yangu nikifa je, nitazikwa kama binadamu wengine? Ndiyo maana nimeamua kujitayarishia jeneza langu,” anasema Scholastica Mhagama (76) mwenye ulemavu wa viungo anayeishi pekee yake katika kibanda kilichoezekwa kwa nyasi.

“Nimetengeneza kabisa jeneza langu siku nikifa wanizike humu. Naomba Mungu anichukue haraka ili kuepukana na mateso haya.

Nimetengwa na jamii na majirani wanashindwa kunisaidia wanadai eti mimi ni mchawi kwa sababu watoto wangu wote wanne walikufa wakiwa wadogo.

Naumia sana kusingiziwa kitu ambacho sikijui,’’ anasema kwa masikitiko. Bibi huyo anasema kuwa aliweza kutengeza jeneza hilo baada ya kupewa Sh40,000 na mfadhili mmoja. “Tayari nilikuwa na mbao kwangu, hivyo kazi ilikuwa kumlipa kijana fedha na kumpa mbao ili anitengenezee jeneza,” anasema.

Source:Mwananchi

Kama bado ujaungana namimi ili kila nikipata habari zikufikie  kirahisi  BONYEZA HAPA 

Umeipata hii ya Weusi kusemekana wamecopy wimbo??

Kupitia You heard ya August 04,Weusi wamesemekana kucopy wimbo na kuurudia kuanzia namna wanavyorap mpaka beat iliyotumika kwenye wimbo huo,Joh Makini kaongea na kapatikana pia producer wa wimbo huo NahReel nae kazungumza.

Bonyeza play kusikiliza PLAY HAPA 

Chanzo millardayo

Picha: Kwa gari jipya na zawadi ya shilingi milioni 250, harusi ya Pastor Myamba ni funika bovu!

Kwa ukubwa wa zawadi aliyopewa, huenda harusi ya Pastor Myamba ikawa harusi ya staa wa Tanzania iliyofana na yenye stunts zaidi.

Muigizaji huyo wa filamu aliukimbia mji wa Dar na kwenda kufungia harusi yake visiwani
Zanzibar ambako hakuishia kualika mastaa wenzie tu, bali pia zawadi alizopewa, zinatosha
kuanzisha kampuni yake nyingine.

Kama bado ujaungana na mimi ili kila nikipata habari zikufikie kirahisi  BONYEZA HAPA 

Mwanamke Aliyejeruhiwa kwa bomu la polisi akatwa kiganja cha mkono wa Kulia

Mkazi wa Mbagala Zakhiem, Mwanaharusi Hamis amepoteza kiganja chake cha mkono wa kulia baada ya kulipuliwa na kitu kinachodaiwa kuwa ni bomu lililorushwa na polisi wakati wakitawanya wananchi.

Mwanaharusi alilipuliwa na bomu hilo Agosti Mosi 2014, saa 3:00 usiku alipokuwa anatoka ndani kwenda msalani.

Akizungumza na mwandishi jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Wodi ya Mwaisela namba mbili alikolazwa, alisema tukio hilo limebadilisha kabisa mustakabali wa maisha yake.

Mwanaharusi, ambaye ni mama wa watoto wawili alisema alikumbwa na madhila hayo wakati polisi walipokwenda mtaani kwao kumkamata mtuhumiwa wa wizi wa pikipiki.

Alisema walipofika, vijana waliokuwa maeneo hayo waliwarushia polisi mawe, ndipo polisi walipofyatua mabomu ya machozi na risasi kuwatanya wananchi hao.

“Ilikuwa saa 3:00 hivi mimi na watoto wangu tukiwa ndani hatujui nini kinachoendelea nje, ghafla tulianza kusikia milio ya risasi na mvumo wa kitu kuelekea upande wa ilipo nyumba yetu. Wakati huo nilikuwa natoka ndani kwenda msalani, nikaona kitu kimenipiga na kunichana sehemu za mkono na miguuni, baadaye nikagundua kilichonipiga kilikuwa bomu,” alisimulia Mwanaharusi.

Alisema baada ya tukio hilo polisi walimpelekea kituoni kwa ajili ya kupata fomu namba ya tatu ya matibabu (PF3) na baadaye Hospitali ya Temeke, alikopewa rufaa ya kwenda Muhimbili kwa kuwa alikuwa akitoka damu nyingi.

“Nimechanganyikiwa. Mimi ndio mtafutaji wa familia, mwanangu wa kwanza amemaliza kidato cha nne na wa pili ana miaka tisa,” alisema.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Temeke, Kienya Kienya alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema ufafanuzi utatolewa leo na kamanda wa Kanda ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova.

Kama bado ujaungana na mimi ili kila nikipata habari zikufikie kirahisi  BONYEZA HAPA 

Heche AMLIPUA January Makamba.....Asema Hana SIFA za kugombea Urais 2015

MWENYEKITI wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA), Bw. John Heche, amemtaka Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Bw. January Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli, mkoani Tanga, kuacha kufikiria urais kwani Watanzania hawataki Rais kijana bali wanahitaji mtu atakayeweza kuongoza nchi.

Bw. Heche aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Shule ya Msingi Sima A, Wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu.

Alisema Bw. Makamba hana sifa za kuwania urais kama anavyoamini kwa kutumia ushawishi wa vijana kupewa nafasi ya kuongoza nchi na kusema Watanzania wanahitaji kiongozi anayeweza kutatua kero zao.

Bw. Heche ambaye alikuwa kwenye ziara ya Oparesheni Sangara inayoendeshwa katika Mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara, alisema Watanzania hawako tayari kuongozwa na Rais kijana.

"Makamba anaposema huu ndio wakati wa vijana kushika urais anapotoka kwani hana sifa hizo....nawaomba vijana jitokezeni kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapigakura ili tuweze kuiondoa CCM madarakani na kukiunga mkono CHADEMA," alisema.

Kama bado ujaungana na mimi ili kila nikipata habari zikufikie kirahisi BONYEZA HAPA 

Mama Ajifungua Watoto WANNE Katika Hospitali 2 kwa siku 2 Tofauti mkoani Mwanza

MKAZI wa Kijiji cha Lupili wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza, Tecla Kazimili (24), amejifungua watoto wanne, watatu wa kike na mmoja wa kiume kwa njia ya kawaida katika hospitali mbili tofauti na siku mbili tofauti.

Katika hospitali ya kwanza, ambayo ni zahanati ya Kijiji cha Lupili Agosti mosi mwaka huu, Tecla alionekana ana ujauzito wa mtoto zaidi ya mmoja ambapo wakati wa kujifungua, alizaliwa wa kiume akiwa na kilo 1.6, lakini kwa bahati mbaya alikufa.

Hata hivyo, wakunga walishuhudia mzazi huyo akiendelea kuwa na dalili ya kujifungua mtoto mwingine, lakini akawa amegoma kupita katika njia.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Marko Mwita, alisema baada ya kutokea kwa hali hiyo, alipigiwa simu kuombwa msaada.

“Baada ya kupokea taarifa hiyo majira ya usiku, nilituma gari la wagonjwa kukimbilia kwenye zahanati hiyo iliyopo umbali wa kilometa 60 na kumleta mama huyo katika Hospitali ya Wilaya kwa huduma zaidi,” alisema.

Alisema alipofikishwa hospitalini hapo, Tecla aliendelea kujifungua mpaka kesho yake hatimaye idadi ya watoto ikafikia wanne.

“Hili ni tukio la kwanza katika hospitali hii ya Wilaya, mtu kujifungua watoto wanne, ni matukio yanayotokea mara chache, lakini tunamshukuru Mungu mzazi anaendelea vizuri huku watoto wake watatu, wote wa kike kila mmoja akiwa na uzito wa kilo mbili,” alisema.

Dk Mwita alisema watoto hao wanahitaji uangalizi na msaada wa hali ya juu, kwani ni rahisi kupata maambukizi. Alitoa mwito kwa jamii kumsaidia mama huyo, kwani watoto hao wanahitaji msaada wa hali na mali kwa kuwa maziwa ya mama pekee hayatawatosheleza.

Akizungumzia historia yake ya uzazi, Tecla alisema watoto hao ni uzazi wake wa nne na katika ule uliopita, watoto wote aliowazaa walifariki dunia katika umri tofauti, lakini wa utoto.

“Kitendo cha watoto kufa baada ya kufikisha umri fulani, kilimfanya mume wangu anifukuze, nikalazimika kurejea nyumbani kwetu ambapo nilipewa ujauzito na kijana mwingine,” alisema.

Alisema wakati anahudhuria kliniki, alielezwa kwamba alikuwa na zaidi ya mtoto mmoja baada ya kutoa taarifa kuwa anaona tabia ya ujauzito huo ni tofauti na uzazi wake uliopita.

“Namshukuru Mungu kwa kunipatia watoto hawa na naiomba Serikali inisaidie kuwatunza ili wakue vizuri kwani peke yangu siwezi,” alisema. Kwa mujibu wa Tecla, aliumwa uchungu kwa siku tatu na alimaliza kujifungua Agosti 2.

Kama bado ujajiunga nami ili kila nikipata habari zikufikie kirahisi  BONYEZA HAPA 

Picha: AY na wasanii wengine wakiwa ikulu ya Marekani, White House

AY ameungana wasanii wengine wakubwa barani Afrika jijini Washington DC, kwa mwaliko kutoka ikulu ya Marekani kuhudhuria mkutano wa viongozi wa Marekani na Afrika utakaofanyika wiki hii.

AY akiwa pamoja na Femi Kuti, VictoriabKimani na wengine

Rais Barack Obama atawakaribisha viongozi kutoka barani Afrika kwenye mji huo mkuu wa Marekani katika mkutano wa siku tatu. Huo ni
mkutano mkubwa zaidi kuwahi kufanyika kati ya Rais wa Marekani na viongozi wakuu wa
nchi mbalimbali za Afrika.

Kwenye ziara hiyo, wasanii hao watakutana na viongozi wa juu wa serikali Marekani, wajumbe wa taasisi ya Young African Leaders Initiative (YALI) na wajumbe wa Congress. Pia watatumbuiza siku ya August 4 ukiwemo wimbo wao wa ‘Cocoa Na Chocolate’.

Kama bado uja ungana na mimi ili kila nikipata habari zikufikie kirahisi  BONYEZA HAPA