Monday, August 11, 2014

Umesikia alichokisema Mke wa Dansa wa Diamond kuhusu anti Ezekiel?kipo hapa.

Wiki iliyopita alisikika Anti Ezekiel akielezea uhusiano wake na Moses Iyobo ambaye ni dansa wa Diamond Platnumz,sasa leo amesikika mpenzi wake ambaye ndiye anaishi nae ambaye kaongea na Soud Brown kuhusu hili jambo. BONYEZA HAPA KUSIKILIZA  Source millarda...

SIMBA SC YAWAPA MIKATABA YA MIAKA MIWILI KILA MMOJA , KWIZERA NA KIONGERA...SASA ‘MAPROO’ WAMETIMIA MSIMBAZI

Wanaungana tena; Paul Kiongera alicheza pamoja na Donald Mosoti Gor Mahia ya KenyaSIKU moja baada ya kuvunja Mkataba na kocha wake, Mcroarta Zdravko Logarusic, Simba SC imewasainisha mikataba ya miaka miwili kila mmoja, kiungo Pierre Kwizera raia wa Burundi na mshambuliaji Mkenya, Paul Kiongera. Simba SC jana ilivunja mkataba na Loga ikiwa ni siku moja tu baada ya timu hiyo kufungwa mabao 3-0 na ZESCO ya Zambia katika mchezo wa kirafiki juzi Uwanja...

RASMI, MANGALA NI MCHEZAJI WA MANCHESTER CITY, AKAMILISHA KILA KITU

KLABU ya Manchester City imethibitisha kukamilisha usajili wa Eliaquim Mangala kutoka Porto, na mchezaji huyo amesema anataka kushinda mataji na mabingwa hao wa England. Man City ambayo inakamilisha usajili wa mchezaji huyo siku moja baada ya kufungwa na Arsenal mabao 3-0 katika mechi ya Ngao ya Jamii, inaaminika wamelipa Pauni Milioni 32 kumpata mchezaji huyo. Beki huyo wa kati atavaa jezi namba 20 Uwanja wa Etihad, na pia amesema kusajiliwa kwa...

KUMBE MANYAUNYAU NI TAPELI: SHAHIDI AELEZEA JINSI WALIVYOTAPELIWA SH 29.6 MIL NA MGANGA HUYO

Dar es Salaam, Shahidi wa pili katika kesi ya kujipatia Sh29.6 milioni kwa njia ya udanganyifu inayomkabili mganga wa jadi, Dunia Salumu (37) ‘Manyaunyau’ amedai kuwa walilazimika kuuza kiwanja na nyumba ya urithi kutafuta fedha za kununua mabeberu saba na mafuta ya ngamia ili kumpa mganga huyo kama masharti ya kumfufua ndugu yao aliyefariki dunia. Manyaunyau alifikishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Desemba mwaka 2013 akikabiliwa...

NEW UPDATES: UNDANI ZAIDI WA KIBONDE WA CLOUDS FM ALIVYOTIWA MBARONI!

Mtangazaji Ephraim Kibonde akidhibitiwa na Polisi wa usalama barabarani maeneo ya Mwenge. WIKIENDI iliyopita haikuwa njema kwa mtangazaji Ephraim Kibonde baada ya kutupwa nyuma ya nondo katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar kwa msala wa kudaiwa kugonga gari na kutoa lugha ya matusi. Kwa mujibu wa chanzo chetu makini cha habari ambacho kimeshuhudia sakata hilo mwanzo mwisho, ishu nzima ilianzia maeneo ya Makumbusho ambapo gari alilokuwa...

KAULI YA ASKOFU KAKOBE MARA BAADA YA GWAJIMA KUNUNUA HELKOPTA

Kama sehemu ya vyanzo vyako vya habari ni mitandao kama vile website, blogs, facebook, twitter na Instagram inawezekana hii stori ya Gwajima ambae ni Muhubiri wa Injili kununua Helikopta uliiona hata zaidi ya mara moja. Hata hivyo Muhubiri mwenzake Askofu Zacharia Kakobe Aug 10 2014 amenukuliwa na gazeti la Nyakati na kuizungumzia hiyo Helikopta akisema ‘kitendo cha Gwajima kununua helikopta kwa ajili ya kazi zake za Injili kinastahili kufurahiwa...

New AUDIO | AT - Sitaki Kusemwa | Download hapa

 BONYA HAPA KUDOWNLOAD &nbs...

New AUDIO | MKUBWA NA WANAWE - NISEME | Download hapa

 BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD&nbs...

TETESI ZA SOKA ZILIZOSHAMILI KWENYE MAGAZETI MBALIMBALI YA ULAYA ZIPO HAPA

Manchester United wametoa dau la pauni milioni 55 kumtaka kiungo wa Real Madrid Angel Di Maria, 26 (Daily Express), United pia watatazama kumchukua kiungo wa zamani wa Arsenal Alex Song, 26, kutoka Barcelona iwapo watashindwa kumpata Arturo Vidal, 27 (Daily Express), Borussia Dortmund wamesema watafanya kila wawezalo kubaki na kiungo wao Marco Reus, 25, licha ya mchezaji huyo kuwindwa na Arsenal, Liverpool na Manchester United (Metro), Manchester...

JE WAJUA KUA NEY NDO CHANZO CHA DIAMOND KUHAIRISHA KUMUOA WEMA??? SOMA CHANZO HAPA

IMEVUJA kwamba Staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ndiye aliyemshauri Nasibu Abdul ‘Diamond’ asioe kwa sasa ili asishuke kimuziki. Staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ Ushauri huo umekuwa mwiba kwa mpenzi wa Diamond, Wema Sepetu ambaye amekuwa na ndoto ya kuolewa na staa huyo anayekimbiza kitaani na wimbo wake wa Mdogomdogo. Akifafanua zaidi kuhusiana na ushauri huo, Nay alisema: “Kuna mifano mingi sana nimeiona...