Monday, August 18, 2014
MAN CITY YAANZA NA MOTO WAKE LIGI KUU ENGLAND
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya England, Manchester City wameanza vizuri harakati za kutetea taji lao, kufuatia ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Newcastle United, Uwanja wa St. James Park.
Katika mchezo huo uliotanguliwa na maombelezo ya Liam Sweeney na John Alder, waliofariki kwenye ajali ya ndege ya MH17, City ilipata bao moja kila kipindi. Alianza kiungo David Silva dakika ya 39, kabla ya mshambuliaji Sergio ‘Kun’ Aguero kupiga la kuhakikisha ushindi dakika ya 90- siku chache baada ya nyota hao wote kusaini mikataba mipya na timu hiyo ya Etihad.
Kikosi cha Manchester City kilikuwa; Hart, Clichy, Kompany, Dimichelis, Kolarov, Toure, Fernando, Nasri/Milner dk77, Jovetic/ Fernandinho dk72, Silva na Dzeko/Aguero dk81. Newcastle United; Krul, Janmaat, Williamson, Coloccini, Dummett, Anita/Obertan dk62, Gouffran/Aarons dk73, Colback, Sissoko, Cabella na Riviere/Perez dk80.
Na mdadidiblog/festo saimon
BONYEZA HAPA KUHUNGANA NA BLOG HII ILI UPATE HABARI MBALIMBALI PUNDE ZINAPOTUFIKIA
Sunday, August 17, 2014
LIVERPOOL YAANZA VYEMA LIGI KUU ENGLAND, WATAKATIFU WAKALIA 2-1 SWAAFI ANFIELD...MAMBO YA STERLING NA STURRID
Shukrani kwake, mshambuliaji wa kimataifa wa England, Daniel Sturridge aliyefunga bao la ushindi dakika ya 79 na kumpa mwanzo mzuri Brenden Rodgers aliyeukosakosa kidogo ubingwa msimu uliopita akizidiwa kete na Manchester City.

Sterling alitangulia kuwafungia Wekundu hao dakika ya 23, kabla ya Nathaniel Clyne kuwasawazishia Watakatifu dakika ya 56.
Kikosi cha Liverpool kilikuwa; Mignolet, Manquillo, Skrtel, Lovren, Johnson, Henderson, Gerrard, Lucas/Allen dk63, Sterling, Coutinho/Lambert dk76 na Sturridge.
Southampton: Forster, Clyne, Fonte, Yoshida, Bertrand, Wanyama, Schneiderlin, Tadic/Long dk73, Ward-Prowse, S Davis/Isgrove dk82 na Pelle.
Katiba Mpya hakieleweki

Dar es Salaam. Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema amesema mchakato wa Katiba Mpya ukikwama kufika mwisho kutokana na mvutano unaoendelea wa makundi mawili kushikilia misimamo yao, kutafanyika marekebisho ya 15 katika Katiba ya sasa ya mwaka 1977 ili kuruhusu kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
Pia, ameipongeza iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa kuandaa Rasimu bora na kuwaomba wajumbe wake kuwa na ngozi ngumu ya uvumilivu katika kipindi hiki na waepuke kurushiana maneno na watu wanaowakejeli.
Jaji Werema aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuelezea mchakato huo ulipotoka, ulipofika na unakokwenda huku akitumia Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na Rasimu ya Katiba kufafanua baadhi ya mambo.
Mwanasheria huyo, akijibu swali aliloulizwa kuwa Bunge Maalumu la Katiba linaendelea wakati wajumbe kutoka Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakiwa hawashiriki, Je, ikishindikana kupatikana kwa theluthi mbili itakuaje? Alisema: “Katika kamati theluthi mbili inatosha, lakini kule mwisho (katika kura ya maoni ya kuipitisha Katiba itakayopendekezwa) kama tutafika darajani, hilo ni suala la siku za usoni.
“Kama tutafika huko na kukuta hakuna pa kutokea, tutarudi bungeni (Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) na kufanya marekebisho ya 15 katika Katiba ya sasa ya mwaka 1977 kama uwepo wa Tume huru ya Uchaguzi, mgombea binafsi na kupunguzwa kwa mamlaka ya Rais, vitu ambavyo vimekuwa vikizungumzwa sana na wananchi,” alisema Jaji Werema.
Kuhusu madaraka ya Rais kulivunja au kulisitisha Bunge hilo, Jaji Werema alisema “Sheria haimruhusu Rais kulivunja au kulisitisha na katika maongezi yangu na yeye (Rais Kikwete) nilimweleza kwamba hana madaraka hayo.”
Aliongeza: “Nimemwambia hana mamlaka ya kusimamisha, hana mamlaka ya kulivunja na wala asifikirie kwani Sheria haikumpa mamlaka na akifanya hivyo atakuwa anavunja Katiba.”
Jaji Werema alisema mamlaka ya Bunge hilo inatokana na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inayolitaka kujadili na kupitisha Rasimu iliyopendekezwa na Tume kisha kuandaa Katiba na kuipeleka kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura ya maoni.
“Kisheria maana ya kujadili ni kuboresha, kubadilisha na kuweka jambo vizuri na hii siyo mimi bali tulikubaliana wote na kanuni zikaandaliwa,” alisema Jaji Werema.
Kuhusu mabadiliko ya kanuni ilizozifanya Bunge hilo wakati Ukawa wakiwa hawapo alisema: “Tulifanya hivyo kwani Rais (Kikwete) amesema siku 60 alizoongeza zikiisha hawezi kuongeza tena, hivyo tumefanya hivyo ili kuwezesha siku hizo zitoshe.”
Aprili 16 mwaka huu, wajumbe wa Ukawa kutoka vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na baadhi ya wajumbe kutoka kundi la 201 walisusia kushiriki shughuli zote za Bunge hilo hadi pale Rasimu iliyowasilishwa na Jaji Warioba iheshimiwe kutokana na kubeba maoni na mapendekezo ya wananchi.
Hata hivyo, Bunge hilo liliendelea na vikao vyake hadi lilipoahirishwa Aprili mwaka huu kupisha Bunge la Bajeti na Agosti 5 mwaka huu. Lilirejea tena na kuanza vikao vyake huku wajumbe wa Ukawa wakiwa wameendelea kushikilia msimamo wao.
Credit mwananchi
Hatimaye Masanja aamua kufungikia ishu ya Diamond na Wema kwa kuwapa ushauri 'mzito'
Baada ya uhusiano wa diamond na wema kuingia katika misukosuko na diamond kutoa ujumbe mzito kumhusu wema sepetu, mchekeshaj maarufu hapa bongo masanja mkandami ameamua kufua ya moyoni kuhusiana na uhusiano wa wawili hawa.
masanja alisema haya “Street pastor anasema.. hili swala la diamond na wema nadhani mungu amemuhurumia mmoja wapo kati ya hao wawili.
kama wangekuwa watu wa kuoana wangesha oana uchumba gani mrefu kama wanasomea udokta???? rafiki yangu nasib, kama kweli mlipendana kwa dhati hizo kasoro zinarekebishika, maana hakuna mwanadamu aliye sahihi kwan hata ww nasib unamapungufu yako. na wewe dada yangu wema lazima ujue mme ndio kichwa cha nyumba kwa maelezo hayo inaonyesha haumsikilizagi mwenzio omba msamaha tenaaa na tena na ukubali kubadilika.
mi sipendi mkiwa mnaongozana wote kwenye ma show ya usiku mme kafanye kazi mke abaki home ukirudi mwili umepoa hata ujauzito unaingiaa!! sasa woote stejini mkirudi miili ya moto si mtazaa popompoo jamaniii!! nitafurahi kusikia tofauti zenu mmezimaliza kwa amani ili mashabiki wenu wasijisikie vibaya.” Alimaliza masanja.!
BOFYA HAPA KUHUNGANA NA BLOG HII ILI UPATE HABARI KIRAHISI PUNDE ZITUFIKIAPO
PERUZI KURASA ZA MBELE NA NYUMA ZA MAGAZETI MBALIMBALI YA LEO JUMAPILI
VAN GAAL ASEMA KIPIGO CHA JANA KITAPOTEZA KUJIAMINI MAN UNITED, AKIRI PIA IPO HAJA YA KUSAJILI, HASWA MABEKI
Bao la Gylfi Sigurdsson dakika ya 72 lilimvuruga kocha mpya wa United, Van Gaal kuftia ushindi mfululizo katika mechi sita za kujiandaa na msimu, Mashetani hao Wekundu wakifungwa kwa mara ya kwanza nyumbani katika mchezo wa ufunguzi ndani ya miaka 42.
"Unaposhinda kila kitu katika wakati wa maandalizi na kuja kufungwa mechi ya kwanza, hiyo haiwezi kuwa mbaya," amesema. "Tumejijengea hali ya kujiamini kwa kiasi kikubwa na kisha itaondoka kwa sababu ya matokeo haya,".’

Mholanzi huyo alilazimika kuwachezesha kwa mara ya kwanza katika Ligi Kuu ya England Jesse Lingard na Tyler Blackett, akiwa amesaini wachezaji wawili tu wapya— Ander Herrera na Luke Shaw msimu huu.
Alipoulizwa kama kipigo hicho kitamlazimu kuingie sokoni kusajili kuboresha kikosi, Van Gaal alisema: "Nilifikiri hivyo mkabla ya mechi hii, hivyo hakuna tofauti. Wakati tunacheza Marekani niliona kama hivyo. Kweli tunahitaji mabeki. Lakini huwezi kusema hivyo, kwa sababu tumepoteza mechi moja na tumeshinda nyingine zote, hiyo ni beki. Ni timu ambavyo tumecheza,".
Katika staili yake maarufu, Van Gaal, Mholanzi hiyo hakumnyooshea kidole yeyote baada ya mechi. Kocha huyo mpya wa United, aliwalaumu wachezaji wake kwa kucheza ovyo. Pia alisema walikosa hali ya kujiamini na hawakucheza kitimu.
"Ni siku mbaya sana kwetu. Imewaangusha sana wachezaji, mashabiki, mimi, na viongozi,"alisema.
Na mdadisiblog/festosaimon