Tuesday, August 12, 2014

BREAKING NEWS: DEREVA WA BASI LA WACHEZAJI WA YANGA AFARIKI DUNIA ASUBUHI HII

Uongozi wa klabu ya Young Africans unasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Dereva wa Bus Kubwa la Wachezaji (Yutong) Bw Maulid Kiula kilichotokea alfajiri ya leo Ilala jijini Dar es salaam.

Taratibu za mazishi zinaendelea nyumbani kwa marehemu mtaa wa Chunya karibu na Bungoni Ilala jijini Dar es salaam.

Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi

MUHIMU SANA: USAILI WA JESHI LA POLISI TANZANIA KWA WAKAZI WA MBEYA

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, BARAKAEL .N. MASAKI – ACP anawatangazia Wananchi wote ya kuwa orodha ya majina ya vijana waliomaliza Kidato cha Nne mwaka 2013 na cha Sita mwaka 2014 na kuchaguliwa kufanya usalii wa kujiunga na Jeshi la Polisi inapatikana kwenye tovuti ya Polisi: www.policeforce.go.tz au wafike ofisi ya kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya iliyopo Forest jirani na Mahakama kuangalia majina yao.

Muhimu:

• Mwombaji anaruhusiwa kufanya usaili kwenye kituo chochote cha usaili kilicho karibu naye kulingana na tarehe zinavyoonesha kwenye jedwali hapo juu ili mradi tu awe amejiridhisha kuwa ni miongoni mwa walioitwa kwenye usaili. Jeshi la Polisi halitahusika na lawama yoyote ile kwa mtu atakayekwenda kwenye kituo cha usaili hali ambapo jina lake si miongoni mwa walioitwa kufanya usaili.

• Mwombaji aliyeitwa kwenye usaili aje na vyeti vyake vyote vya masomo [(Academic Certificate(s)/Results slip(s) & Leaving certificate(s) ], nakala halisi ya cheti cha kuzaliwa (Original Birth certificate). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.

• Mwombaji awe na namba ya simu itakayotumika kumjulisha endapo atachaguliwa..

• Kila mwombaji aliyeitwa kwenye usaili atajigharamia usafiri, chakula na malazi kwa muda wote wa zoezi la usaili. Pia waombaji waje na kalamu za wino kwa ajili ya usaili wa kuandika.

Ni muhimu sana kwa kila mwombaji kuzingatia muda wa kuanza usaili.

TAREHE YA USAILI KWA MKOA WA MBEYA NI 28.09.2014 HADI
01.10.2014. SAA 08:00 ASUBUHI HADI 10:00 JIONI.

Na mdadisiblog/festo saimon

 BONYEZA HAPA KAMA BADO UJAJIUNGA NASI 

Mkali wa movie Robin William akutwa amefariki ndani ya nyumba yake

Robin William ni star aliyeanza kupata mafanikio akifanya kazi kama stand up comedian na baadae kuanza kuonekana kwenye movie.

Akiwa na miaka 63 Robin amefariki dunia kwa kifo ambacho hadi sasa hakijajulikana chanzo chake lakini tetesi zinasema kuna uwezekanao kwamba Robin alijiua.

Mwili wake umekutwa nyumbani kwake huko Tiburon California na watu wa karibu wanasema alikuwa anasumbuliwa na msongo wa mawazo hivi karibuni.

Enzi za uhai wake aliwai kushiriki kwenye movie kama The Fisher King,Good will Hunting,Jumanji,Popeye na nyingine. Pia alishinda tuzo kama Academy,Golden Globe,Emmy,Grammy na nyinginezo kwa wakati tofauti.

 KAMA BADO UJAJIUNGA NASI BONYEZA HAPA 

Huu ndiyo usajili wa timu za Ligi Kuu za England

Romelu Lukaku amehamia jumla Everton toka Chelsea
Fillipe Luis (mbele) amehamia Chelsea
Didier Drogba amerejea Chelsea
Kipa David Ospina ametua Arsenal
Luke Shaw ametua Manchester United toka Southampton
Alexis Sanchez ametua Arsenal toka Barcelona

ARSENAL
WALIOSAJILIWA
Alexis Sanchez (Barcelona, £30m),
Calum Chambers (Southampton, £12m),
Mathieu Debuchy (Newcastle, £10m),
David Ospina (Nice, £3m)

WALIOONDOKA
Thomas Eisfeld (Fulham, ada haikutajwa),
Bacary Sagna (Manchester City, huru),
Lukasz Fabianski (Swansea, huru),
Nicklas Bendtner (ameruhusiwa),
Park Chu-young (ameruhusiwa),
Chuks Aneke (ameruhusiwa),
Daniel Boateng (ameruhusiwa),
Wellington Silva (Almeria, mkopo),
Carl Jenkinson (West Ham, mkopo)

ASTON VILLA
WALIOSAJILIWA
Philippe Senderos (Fulham, huru),
Joe Cole (West Ham, huru),
Tom Leggett (Southampton, ada haikutajwa),
Isaac Nehemie (Southampton, ada haikutajwa)
Kieran Richardson (Fulham, ada haikutajwa)

WALIOONDOKA
Marc Albrighton (Leicester City, huru),
Nathan Delfouneso (Blackpool, huru),
Jordan Bowery (Rotherham, ada haikutajwa),
Nicklas Helenius (Aalborg, mkopo),
Yacouba Sylla (Kayseri Erciyesspor, mkopo)

BURNLEY
WALIOSAJILIWA
Lukas Jutkiewicz (Middlesbrough, £2.5m),
Michael Kightly (Stoke, ada haikutajwa),
Marvin Sordell (Bolton, huru),
Matt Gilks (Blackpool, huru),
Matt Taylor (West Ham, huru),
Steven Reid (West Brom, huru)

WALIOONDOKA
Chirs Baird (West Brom, huru),
Junior Stanislas (Bournemouth, huru),
David Edgar (Birmingham, huru),
Keith Treacy (ameruhusiwa),
Brian Stock (ameruhusiwa),
Nick Liversedge (ameruhusiwa)

CHELSEA
WALIOSAJILIWA
Cesc Fabregas (Barcelona, £30m),
Diego Costa (Atletico Mdrid, £32m),
Mario Pasalic (Hadjuk Split, ada haikutajwa),
Filipe Luis (Atletico, £16m),
Didier Drogba (Galatasaray, huru)

WALIOONDOKA
David Luiz (Paris Saint-Germain, £50m),
Romelu Lukaku (Everton, £28million),
Samuel Eto'o (ameruhusiwa),
Frank Lampard (New York City, huru),
Sam Hutchinson (Sheffield Wednesday, huru),
Mark Schwarzer (ameruhusiwa),
Henrique Hilario (ameruhusiwa),
Wallace (Vitesse Arnhem, mkopo),
Bertrand Traore (Vitesse Arnhem, mkopo)
Thorgan Hazard (Borussia Monchengladbach, mkopo),
Ashley Cole (Roma, £1.5m),
Demba Ba (Besiktas, £8m),
Mario Pasalic (Elche, mkopo)
Patrick van Aanholt (Sunderland, ada haikutajwa),
Ryan Bertrand (Southampton, mkopo),
Gael Kakuta (Rayo Vallecano, mkopo)

CRYSTAL PALACE
WALIOSAJILIWA
Chris Kettings (Blackpool, huru)
Fraizer Campbell (Cardiff, £800k)

WALIOONDOKA
Jonathan Parr (Ipswich, huru),
Dean Moxey (Bolton, huru),
Aaron Wilbraham (Bristol City, huru),
Kagisho Dikgacoi (Cardiff, huru),
Danny Gabbidon (ameruhusiwa),
Neil Alexander (ameruhusiwa),
Ibra Sekajja (ameruhusiwa),
Alex Wynter (Portsmouth, mkopo),
Kwesi Appiah (Cambridge, mkopo),
Jose Campana (Sampdoria, ada haikutajwa),
Jack Hunt (Nottingham Forest, mkopo)

EVERTON
WALIOSAJILIWA
Romelu Lukaku (Chelsea, £28m),
Gareth Barry (Manchester City, free)
Muhamed Besic (Ferencvaros, £4m)

WALIOONDOKA
Apostolos Vellios, (Lierse, huru)
Mason Springthorpe (ameruhusiwa)
Magaye Gueye (Millwall, huru)

HULL
WALIOSAJILIWA
Robert Snodgrass (Norwich, £8m),
Jake Livermore (Tottenham, £6m),
Tom Ince (Blackpool, free),
Harry Maguire (Sheffield United, £2.5m),
Andrew Robertson (Dundee United, £2.85m)

WALIOONDOKA
Matty Fryatt (Nottingham Forest, huru),
Cameron Stewart (Ipswich, huru),
Robert Koren (ameruhusiwa),
Abdoulaye Faye (ameruhusiwa),
Conor Henderson (Crawley, huru),
Dougie Wilson (released),
Conor Townsend (Dundee United, mkopo),
Joe Dudgeon (Barnsley, mkopo)

LEICESTER CITY
WALIOSAJILIWA
Matthew Upson (Brighton, huru),
Marc Albrighton (Aston Villa, huru),
Leonardo Ulloa (Brighton, £7m),
Ben Hamer (Charlton, huru),
Jack Barmby (Manchester United, huru),
Louis Rowley (Manchester United, huru)

WALIOONDOKA
Lloyd Dyer (Watford, huru),
Neil Danns (Bolton, huru),
Sean St Ledger (ameruhusiwa),
Zak Whitbread (Derby, huru),
Paul Gallagher (Preston, mkopo),
Marko Futacs (ameruhusiwa),
George Taft (Burton Albion, huru)

LIVERPOOL
WALIOSAJILIWA
Adam Lallana (Southampton, £23m),
WALIOONDOKA
Luis Suarez (Barcelona, £75m),
Luis Alberto (Malaga, mkopo),
Iago Aspas (Sevilla, mkopo),
Andre Wisdom (West Brom, mkopo),
Divock Origi (Lille, mkopo)

MANCHESTER CITY
WALIOSAJILIWA
Fernando (Porto, £12m),
Bacary Sagna (Arsenal, free),
Willy Caballero (Malaga, £6m),
Bruno Zuculini (Racing Club, £1.5m)

WALIOONDOKA
Costel Pantilimon (Sunderland, huru),
Joleon Lescott (West Brom, huru)
Gareth Barry (Everton, huru),
Alex Nimely (ameruhusiwa),
Rony Lopes (Lille, mkopo),
Emyr Huws (Wigan, mkopo)

MANCHESTER UNITED
WALIOSAJILIWA
Luke Shaw (Southampton, £31.5m),
Ander Herrera (Athletic Bilbao, £29m),
Vanja Milinkovic (FK Vojvodina, ada haikutajwa)

WALIOONDOKA
Alexander Buttner (Dinamo Moscow, £5.6m),
Rio Ferdinand (QPR, huru),
Nemanja Vidic (Inter Milan, huru),
Federico Macheda (Cardiff City, huru),
Jack Barmby (Leicester, huru),
Louis Rowley (Leicester, huru)
Ryan Giggs (amestaafu),
Patrice Evra (Juventus, £2.5m)
Bebe (Benfica, £2.4m)

NEWCASTLE
WALIOSAJILIWA
Remy Cabella (Montpellier, £12m),
Emmanuel Riviere (Monaco, £6m),
Siem de Jong (Ajax, £6m),
Daryl Janmaat (Feyenoord, £5m),
Ayoze Perez (Tenerife, £1.5m),
Jack Colback (Sunderland, huru)

WALIOONDOKA
Mathieu Debuchy (Arsenal, £10m),
James Tavernier (Wigan, ada haikutajwa,
Dan Gosling (Bournemouth, huru),
Shola Ameobi (ameruhusiwa),
Conor Newton (Rotherham, huru),
Michael Richardson (ameruhusiwa),
Sylvain Marveaux (Guingamp, mkopo)

QUEENS PARK RANGERS
WALIOSAJILIWA
Rio Ferdinand (Manchester United, huru),
Steven Caukler (Cardiff, £8m)

WALIOONDOKA
Tom Hitchcock (Mk Dons, huru),
Aaron Hughes (Brighton, huru)
Stephane Mbia (ameruhusiwa),
Andrew Johnson (ameruhusiwa),
Luke Young (ameruhusiwa),
Hogan Ephraim (ameruhusiwa),
Angelo Balanta (ameruhusiwa),
Yossi Benayoun (Maccabi Haifa, ada haikutajwa),
Esteban Granero (Real Sociedad, ada haikutajwa)

SOUTHAMPTON
WALIOSAJILIWA
Dusan Tadic (Twente, £10.3m),
Graziano Pelle (Feyenoord, £8m),
Ryan Bertrand (Chelsea, loan)

WALIOONDOKA
Luke Shaw (Manchester United, £31.5m),
Rickie Lambert (Liverpool, £4m),
Adam Lallana (Liverpool, £23m)
Guly do Prado (released),
Lee Barnard (Southend, huru),
Jonathan Forte (released),
Danny Fox (Nottingham Forest, huru),
Andy Robinson (Bolton, huru),
Tom Leggett (Aston Villa, ada haikutajwa),
Isaac Nehemie (Aston Villa, ada haikutajwa)
Dejan Lovren (Liverpool, £20m)
Calum Chambers (Arsenal, £12m)

STOKE CITY
WALIOSAJILIWA
Mame Biram Diouf (Hannover, huru),
Dionatan Teixeira (Banska Bystrica, ada haikutajwa),
Phil Bardsley (Sunderland, huru),
Steve Sidwell (Fulham, huru),
Bojan Krkic (Barcelona, ada haikutajwa)

WALIOONDOKA
Michael Kightly (Burnley, ada haikutajwa),
Matthew Etherington (ada haikutajwa),
Juan Agudelo (ada haikutajwa)

SUNDERLAND
WALIOSAJILIWA
Billy Jones (West Brom, huru),
Jordi Gomez (Wigan, huru),
Costel Pantilimon (Manchester City, huru)
Patrick van Aanholt (Chelsea, ada haikutajwa)

WALIOONDOKA
Jack Colback (Newcastle, huru),
Craig Gardner (West Brom, huru),
Phil Bardsley (Stoke, huru),
Billy Knott (Bradford, huru)
Keiren Westwood (Sheffield Wednesday, huru),
Carlos Cuellar (ameruhusiwa),
Andrea Dossena (ameruhusiwa),
Louis Laing (ameruhusiwa),
Oscar Ustari (Newell's, huru),
David Vaughan (Nottingham Forest, huru),
John Egan (Gillingham, huru),
Ignacio Scocco (Newell's, £800,000)

SWANSEA
WALIOSAJILIWA
Marvin Emnes (Middlesbrough, £1.5m),
Bafetimbi Gomis (Lyon, huru),
Lukasz Fabianski (Arsenal, huru),
Stephen Kingsley (Falkirk, ada haikutajwa),
Gylfi Sigurdsson (Tottenham, ada haikutajwa)
Jefferson Montero (Monarcas Morelia, £4m)

WALIOONDOKA
Leroy Lita (ameruhusiwa),
David Ngog (ameruhusiwa),
Daniel Alfei (Northampton, mkopo),
Jernade Meade (ameruhusiwa),
Darnel Situ (ameruhusiwa),
Michu (Napoli, mkopo),
Ben Davies (Tottenham, £10m)
Michel Vorm (Tottenham, £5m)
Alejandro Pozuelo (Rayo Vallecano, ada haikutajwa)

TOTTENHAM
WALIOSAJILIWA
Ben Davies (Swansea, ada haikutajwa Lazar Markovic WALIOONDOKA
Jake Livermore (Hull, £6m),
Heurelho Gomes (Watford, huru),
Cameron Lancaster (ameruhusiwa),
Alex Pritchard (Brentford, mkopo),
Gylfi Sigurdsson (Swansea, mkopo)

WEST BROMWICH ALBION
WALIOSAJILIWA
Brown Ideye (Dynamo Kiev, £10m),
Craig Gardner (Sunderland, huru),
Joleon Lescott (Manchester City, huru),
Chris Baird (Burnley, huru),
Sebastien Pocognoli (Hannover 96, ada haikutajwa),
Andre Wisdom (Liverpool, mkopo)

WALIOONDOKA
Liam Ridgewell (Portland Timbers, huru),
Billy Jones (Sunderland, huru),
Steven Reid (Burnley, huru),
Cameron Gayle (Shrewsbury, huru),
Diego Lugano (ameruhusiwa),
Zoltan Gera (ameruhusiwa),
Scott Allan (ameruhusiwa),
Nicolas Anelka (ameruhusiwa),
George Thorne (Derby County, ada haikutajwa)

WEST HAM
WALIOSAJILIWA
Enner Valencia (Pachuca, £12m),
Cheikhou Kouyate (Anderlecht, £7m),
Mauro Zarate (Velez Sarsfield, ada haikutajwa),
Aaron Cresswell (Ipswich, ada haikutajwa),
Diego Poyet (Charlton, ada haikutajwa),
Carl Jenkinson (Arsenal, huru)

WALIOONDOKA
Joe Cole (Aston Villa, huru),
Matt Taylor (Burnley, huru),
Stephen Henderson (Charlton, huru),
Jack Collison (ameruhusiwa),
George McCartney (ameruhusiwa),
Callum Driver (ameruhusiwa),
Jordan Spence (ameruhusiwa), (Benfica, £20m),
Emre Can (Bayer Leverkusen, £9.8m),
Rickie Lambert (Southampton,

By mdadisiblog/festo saimon

 KAMA BADO UJAJIUNGA NASI BONYA HAPA ILI KILA NIKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI 

MARADONA AMCHAPA KIBAO MWANDISHI WA HABARI.

Gwiji la soka ulimwenguni Diego Maradona ameibuka na skendo nyingine nchini Argentina baada ya kumzaba kibao mwandishi mmoja wa habari ambaye inasemekana alimsemea maneneo machafu mke wa zamani wa gwiji huyo. Kitrndo hicho kilimuhudhi Maradona ambaye alikuwa safarini pamoja na mtoto wake.

 ASANTE NA KALIBU TENA ILA KAMA BADO UJAJIUNGA NASI BONYA HAPA 

DIAMOND PLATNUM- ”MRISHO NGASSA NDIYE MWANASOKA PEKEE NINAYEMFAHAMU TANZANIA”

Mwanamuziki wa Bongo Flovour Nchini Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platinums, amesema hajaridhilika na alipo sasa kimuziki, ndio maana kila siku anajifunza kwa kufuatilia kwa ukaribu maisha ya Nyota wengi hasa wanamichezo Kutoka Mataifa Tofauti Duniani.

Diamond ambae ni miongoni mwa wanamuziki waliofanya vyema kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta Mkoani Mwanza hivi karibuni, ametoa taarifa za kuwafuatilia nyota hao mbalimbali kwenye mahojiano maalum na Shaffih Dauda, kupitia Dauda TV. Miongoni mwa nyota ambao Diamond anawafuatilia hasa kupitia Mtandao wa Instagram, ni Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Cameroon Samuel Etoo, Kiungo Mshambuliaji wa Brazil na Barcelona Neymar, Bondia Mmarekani Floyd Myweather na wengineo.

Pamoja na Diamond kuweka hilo wazi, pia amesema aliwahi kucheza masumbwi, kisha akahamia kwenye Soka hasa nafasi ya golikipa na namba sita yaani kiungo Mkabaji, lakini aliamua kuachana na Soka baada ya mama yake kumsii kufanya hivyo kwa muda mrefu.

Awali kulikuwa na hisia kwamba Diamond anashabikia timu ya Dar-es- salaam Young Africans, hasa baada ya kuweka picha kwenye mitandao akiwa na Mrisho Ngasa mara kadhaa, lakini amesema yeye na Ngasa ni marafiki, na sio mshabiki wa Yanga kama inavyodhaniwa.

Diamond ameongeza kwa kusema sio tu haishabikii Yanga, bali kwa hapa nyumbani hana timu anayoishabikia, badala yake anaipenda FC Barcelona ya Hispania, ambapo amesema kunakipindi mapenzi yalizidi kwa timu hiyo, kiasi cha kuweza kupanga kikosi chote.

 BONYEZA HAPA KUHUNGANA NASI ILI KILA TUKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI 

Credit: dauda

MBEYA YAKIONA CHA MOTO KWA WATOTO WA TMK AIRTEL RISING STARS

TIMU ya wavulana ya Temeke jana imeyaanza vyema mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa kwa kuifunga Mbeya 2-1 katika mchezo wa ufunguzi uliochezwa kwenye uwanja wa kumbu kumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.

Baada ya kosa kosa za hapo na pale kutoka pande zote mbili, Temeke walifanikiwa kuandika bao lao la kwanza katika dakika ya 27 kupitika kwa mshambuliaji machachali Siaba Selehe.

Bao hilo lilipokelewa kwa nderemo na vifijo na mashabiki wa Temeke. Mshambuliaji wa wa timu ya vijana ya Temeke, Siaba Salehe (jezi nyekundu) akiwania mpira na kipa wa timu ya vijana ya Mbeya, Kelvin Dismas (kulia) na beki Yusufu Hongoli katika mchezo wa mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila upande ukitafuta goli na Mbeya waliweza kusawazisha katika dakika ya 50 kupitia kwa Mantony Malewa aliyefanya kazi ya ziada kupangua ngome ya Temeke na kuweka mpira kimiani.

Goli hilo liliongeza kasi ya mchezo huku Temeke wakisaka goli la kuongoza kwa udi na uvumba na juhudi zao zilifanikiwa kuzaa matunda katika dakika ya 70 kupitia kwa Said Mussa.

Katika mechi ya wasichana ya fungua dimba ya wasichana, timu ya Ilala ilifanya mauji ya kuungamiza baada ya kuifunga Mwanza 6-0. Dalili za kupoteza mchezo huo kwa vijana wa Mwanza ilianza kuonekana mapema ambapo Ilala walipata goli la kwanza katika dakika ya sita kupitia kwa Rehema Abdul ambaye alifunga manne peke yake.

Abdul alifunga magoli mengine katika dakika za 38, 47 na 67 huko magoli megine yakigungwa na Arasa Abdul katika dakika za 56 na 65. Kwa ujumla Ilala walitawala mchezo katika kila idara.

Mechi nyingine zilizotarajiwa kuchezwa jana ni kati ya Zanzibar na Temeke (wasichana) na Ilala dhidi ya Mwanza (Wavulana). Mashindano hayo ya kubaina na kuendeleza vipaji ngazi ya Taifa yalitarajiwa kufunguliwa rasmi na Mjumbe wa Heshima wa shirikisho la soka la Afrika (CAF) Said El Maamry.

Wachezaji 32 watachaguliwa katika mashindano haya ili kuunda timu za wasichana na wavulana ili kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars itakayofanyika nchini Gabon baadaye mwezi huu.

 HABARI ZINGINE ZIPO HAPA BONYA UZIONE 

KOCHA KIBOKO YA YANGA AWASILI DAR KUMWAGA WINO NA WEKUNDU WA MSIMBAZI

Na Princess Asia, DAR ES SALAAM KOCHA bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2009/2010, Patrick Phiri anatarajiwa kutua Dar es Salaam Ijumaa wiki hii kwa ajili ya kusaini Mkataba wa kuifundisha klabu yake ya zamani, Simba SC.

Mzaliwa huyo wa Mei 3 mwaka 1956, alifanya kazi kwa awamu tatu tofauti akiwa na Wekundu hao wa Msimbazi kati ya mwaka 2004 na 2010 na kwa mafanikio makubwa- na sasa anataka kurejesha enzi. Mzambia huyo alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu akiwa na Simba SC, misimu ya 2004/2005 na 2009/2010 na pia alishinda Makombe ya Tusker mwaka 2005 la Tanzania na Kenya.

Mazungumzo yamekwishanyika na makubaliano yamefikiwa baina ya Phiri na Simba SC na sasa atakuja kufanya kazi tena Msimbazi, akisaidiwa na Nahodha wake enzi zake akifundisha timu hiyo, Suleiman Abdallah Matola ‘Osama’.

Phiri ni kocha anayekubalika zaidi mbele ya mashabiki wa Simba SC miongoni mwa makocha waliowahi kufundisha klabu hiyo- rekodi yake ya kukumbukwa zaidi ikiwa ni kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2009/2010 bila kufungwa hata mechi moja.

Lakini pia, namna alivyoweza kuiongoza Simba SC kuwatambia watani wa jadi, Yanga SC ni jambo lingine linalomfanya awe kocha mwenye heshima ya kipekee Msimbazi. Katika awamu zote tatu alizofundisha Simba SC awali, Phiri hajawahi kufukuzwa- kwani amekuwa akiondoka mwenyewe kwa sababu mbalimbali.

Kwa sasa, mume huyo wa Cecilia Mutale waliyezaa naye watoto wawili, Melesianiah na Patrick Junior, anarejea Simba SC akitokea Green Buffaloes ya Ligi Kuu ya Zambia.

Phiri ni kocha mwenye mafanikio tangu anacheza soka katika klabu za Rokana United (sasa Nkana F.C.) na Red Arrows zote za nyumbani kwao, Zambia kama mshambuliaji. Alikuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Zambia kilichocheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 1978 na 1982, kabla ya kuiwezesha Chipolopolo kufuzu kwa AFCON ya mwaka 2008 nchini Ghana.

Akiwa kocha, Phiri pia aliiongoza timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Zambia kucheza Fainali za kwanza kabisa za Kombe la Dunia nchini Nigeria mwaka 1997 kabla ya kushinda tuzo ya kocha bora wa mwaka nchini mwake mwaka 1999.

Simba SC juzu ilivunja mkataba na Mcroatia, Zdravko Logarusic ikiwa ni siku moja tu baada ya timu hiyo kufungwa mabao 3-0 na ZESCO ya Zambia katika mchezo wa kirafiki juzi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Loga ambaye aliongezewa Mkataba wa mwaka mmoja mwezi uliopita- inadaiwa amefukuzwa kwa sababu za kutotii miiko na maadili ya klabu na Rais wa klabu hiyo, Evans Aveva alisema jana kwamba uamuzi huo umekuja baada ya kumvumilia kwa kiasi cha kutosha.

Loga ameondoka Simba SC baada ya kuiongoza katika mechi 21 tangu Desemba mwaka jana, kati ya hizo akishinda nane, sare tano na kufungwa nane.

Loga aliyerithi mikoba ya Mzalendo, Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’, aliikuta Simba SC bado ipo kwenye mbio za ubingwa msimu uliopita, lakini mwishowe ikamaliza nafasi ya nne nyuma ya Mbeya City, Yanga SC na Azam FC mabingwa.

 KAMA UNATAKA KILA HABARI NIKIPATA ZIKUFIKIE KIRAHISI BONYA HAPA 

JE NIKWELI JOKATE ANAPENDA KUIGA MASTAA WA MAMTONI?!!! CHEKI PICHA HIZI

Urembo ni kitu kizuri na kwenda na Fasheni ndio msingi wakuonekana HOT kila wakati...mwanadada Jokate hayuko nyuma kwenda sambamba na wakali wa nje...big up!!!...umeziona  picha hizo  ni kwajinsigani anavyokwenda nao kwenye upande wa NYWELE!!!

PICHA ZA WEMA NA DIAMOND WAKILA GOOD TIME ZIWANI JIJINI MWANZA!!!