Sunday, September 21, 2014
 |
| Wanakwaya wa Kanisa la Tanzania
Assemblies of God, Hanipher na Godfrey
(mtoto wa mchungaji) walionaswa wakiwa
kichakani.
kama nimeokooka, utantambuaje kama
namuheshimu Mungu…”
Wimbo huu wa Injili ulioimbwa na Bony
Mwaitege wengi hupenda kuusikiliza kama
burudani lakini una ujumbe mzito hasa
kwa wale wanaosema wameokoka.Hivi
karibuni mjini Iringa, wanakwaya wawili
wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God,
mwanamke alijitambulisha kwa jina moja
la Hanipher na mwanaume aliyesema
anaitwa Godfrey, walinaswa usiku
kichakani katika mazingira yaliyojaa utata,
Risasi Jumamosi linakupa kisa kamili.
Tukio hilo la kushangaza, lilijiri kwenye
eneo la Makanyagio ambalo lina makaburi
ya awali katika Manispaa ya Iringa licha
ya kuwepo na nyumba za wenyeji pia. Kwa
mujibu wa chanzo chetu,
wanakwaya hao walinaswa na sungusungu
ambao siku za hivi karibuni wamekuwa
wakifanya ‘patroo’ katika eneo hilo na la
Isoka kufuatia kuwepo kwa matukio ya
wakazi wake kuvamiwa, kupigwa na
kuporwa mali. Siku ya tukio, sungusungu
hao wakiwa katika majukumu yao
waliwaona wanakwaya hao wakiacha njia
kuu na kuchepukia porini umbali
unaokadiriwa kuwa mita 20 kutoka
barabarani.
“Ilibidi sungusungu wawafuate hadi kule
kichakani, ndipo walipowakuta katika
mazingira tata na yenye maswali mengi
bila majibu. Mbaya zaidi, yule mwanamke
alikuwa na mtoto wa mwaka mmoja
mgongoni,” kilisema chanzo chetu.BOFYA APO CHINI KUSOMA
ZAIDI>> |
BOFYA HAPA
null
0 comments:
Post a Comment