Monday, September 15, 2014
 |
| Mtandao wa Instagram unaohusisha uwekaji
picha umeendelea kupata
mashabiki wengi nchini Tanzania lakini wengi
kati ya watumiaji hao
wameisababisha kuwa kati ya nchi
zinazoongoza kwa matumizi mabaya ya
mtandao huo duniani kote.
Ripoti hiyo imetolewa na Meneja Mawasiliano
wa Mamlaka ya Mawasialiano Tanzania (TCRA),
Innocent Mungy katika mahojiano maalum
aliyofanya na Ibrahim Issa wa 100.5 Times
Fm.
“Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo
zimeongoza kwa watu kulalamika kwamba
matumizi yetu hayaendani na makusudio. Na
hii inatokana na pale watu ambao
wanawafuata watu wa` Tanzania kuona vitu
wanavyoweka vitu wanavyoweka, ugomvi,
matusi, picha za ajabu…za ngono na nini. Sasa
watu huwa wanalalamika.” Amesema Innocent
Mungy.
“Wanapolalamika, ule mtandao huwa unaweka
record kwamba watu wengi waliolalamika
kwenye mtandao huu kuhusu picha za
watumiaji ambao wako Tanzania labda ni 20
wakilinganisha na sehemu nyingine ambazo
idadi inakuwa ndogo zaidi.” Ameongeza.
Amefafanua kuwa kwenye mitandao yote ya
kijamii, wakati wa kujiunga mtumiaji hupewa
maelezo ya kurasa kadhaa kuhusu namna ya
kutumia mtandao huo ikiwa ni pamoja na
makatazo lakini watumiaji wengi wa Tanzania
huwa hawayafuatilii/huyapuuza.
Mwisho, Mungy ametoa wito kwa watumiaji
wa mitandao ya kijamii nchini kuitumia
mitandao hiyo kwa maendeleo na sio
vinginevyo.
“Mitandao hii ya kijamii kama mawasiliano ni
maendeleo. Matumizi ya mitandao sio mabaya
ila watumiaji ndio wanafanya vitu vibaya.
Ningewataka watanzania ambao wanatumia
mawasiliano haya vibaya waache. Tuitumie
vizuri. Na wale watu ambao unawaona wewe
hawaendani na matumizi ambayo
yanapendeza, wafute kwenye mtandao wako.
Wa-Unlike, wa-Unfriend au wa-delete kabisa
ili usione hayo mambo yao ya kipuuzi
wanayofanya.” |
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment