Dili limakamilika: Toni Kroos amesaini mkataba na klabu ya Real Madrid kwa dau la paundi milioni 24 kutokea klabu ya Bayern Munich.
TONI Kroos amekamilisha uhamisho wa paundi milioni 24 kujiunga na klabu ya Real Madrid ya Hispania kutoka kwa mabingwa wa Bundesliga, Bayern Munich.
Mabingwa hao wa Ujerumani wametangaza leo asubuhi kuwa wamefikia makubaliano ya pande zote mbili na nyota huyo anaondoka muda wowote.
Mkataba wa Kroos ulikuwa unamalizika majira ya kiangazi mwakani na mshindi huyo wa kombe la dunia amesaini mkataba wa miaka sita katika dimba la Santiago Bernabeu.
Kama bado ujaungana na page yako ya kimichezo ili kila nikipata habari zikufikie kirahisi BONYEZA HAPA
UKIONA TUKIO LOLOTE USISITE KUTUTUMIA PICHA WHATSAPP NO:06570352125 Festo saimon







0 comments:
Post a Comment