Thursday, July 17, 2014

ARSENAL CHELSEA ZAFANYIANA UMAFIA USAJILI WA SAMI KHEDIRA, WAKALA AMWAGA MCHELE KWEUPE"

Anatimka: Sami Khedira hajasaini mkataba na klabu yake ya Real Madrid na yuko mbioni kuondoka.

KLABU ya Chelsea imepata nguvu ya kupambana kumsajili Sami Khedira baada ya jumatano usiku wakala wa mchezaji huyo kusema hakuna dili lolote lililokamilika na Asernal.

Kocha wa Blues, Jose Mourinho alimsajili beki wa kushoto  Filipe Luis jana kutokea klabu ya Atletico Madrid kwa dau la paundi milioni 18 na sasa ametua nyavu zake kwa Mjerumani Khedira.
Ilifahamika kuwa Arsenal wamekubaliana ada ya uhamisho ya paundi milioni 20 na Real Madrid ili kuinasa saini ya nyota huyo mwenye miaka 27, lakini walikuwa wanahangaikia suala la mshahara ambapo mchezaji huyo anahitaji paundi laki moja na elfu themanini kwa wiki.

Hata hivyo, wakala wa  Khedira, Jorg Neubauer alisema: "Hatuko kwenye mazungumzo na Arsenal. Sidhani kama makubaliano ya ada yanaweza kufanyika, vinginevyo ningekuwa nimeambiwa."

"Khedira anapendwa na Mourinho tangu wakati huo yupo Real Madrid na kocha huyo anaeleweka hivyo. Hilo pia limehamia akiwa Chelsea".
Khedira yupo tu kutokana na wawakilishi wa Real Madrid na mchezaji kushindwa kufikia makubaliano ya kuongeza mktaba.
Neubauer aliongeza:

"Tupo katika mzungumzo na Real Madrid kuhusu mkataba, lakini hakuna kinachokaribia kuamuliwa. Sami amerudi kutoka kombe la dunia na amekwenda likizo".
Source matukiotz
Kama bado ujaungana na mimi ili kila habari za michezo nipatapo zikufukie kirahisi BONYEZA HAPA 


UKIONA TUKIO LOLOTE USISITE KUTUTUMIA PICHA WHATSAPP NO:06570352125 Festo saimon

0 comments:

Post a Comment