Tuesday, September 30, 2014
 |
| Pamoja na H.Baba kuwahi kudai kuwa hana tena
beef na Diamond Platnumz, kuna kila ishara kuwa
mafahari hao wawili bado hawawezi kukaa
kwenye zizi moja. Kama umesahau, wacha
tukukumbushe; Wasanii hao wawili wamewahi
kuingia kwenye beef zito baada ya H.Baba
kumtuhumu Diamond amemuibia wimbo wake
‘Sitaki Kulewa’.
H.Baba akipokea tuzo alizoandaa mwenyewe
So, Jumamosi iliyopita, H.Baba na mke wake,
Flora Mvungi waliandaa tuzo zao wenyewe
ambazo tofauti na vile wengi wanavyodhani, tuzo
hizo zilikuwa serious kabisa kwa kuhusisha watu
muhimu kwenye tasnia ya burudani Tanzania,
waandishi wa habari na pia kutolewa trophy na
fedha taslimu kwa washindi.
H.Baba alijipa tuzo ya ‘Mtumbuizaji Bora’ na
tunafahamu kuwa Diamond Platnumz ni mshindi
wa kipengele cha ‘Mtumbuizaji bora wa kiume wa
muziki’ kwenye tuzo za KTMA 2013. H.Baba
anataka title yake kutoka kwa Diamond? |
 |
| Diamond alishinda tuzo 7 mwaka jana kwenye
KTMA ikiwemo ya Mtumbuizaji Bora
Haya ni maneno aliyosema wakati akipokea tuzo
hiyo:
“Tuzo hii hapa ni ya mtumbuizaji bora Tanzania,”
alisema muimbaji huyo. “Mimi nina tuzo ya East
Africa mtumbuizaji bora, Tanzania sina hata tuzo
moja kwa sababu ya nini nimeshatangaza
naanzisha hii tuzo kwa akili timamu na wala
sivuti bangi. Mimi sivuti sigara wala sinywi
pombe, kama kuna msanii anaona hii tuzo sio
halali yangu mimi ajitokeze. Promota yoyote
ajitokeze huyo msanii alipwe pesa mimi nita-
perform bure na awadhihirishie watanzania
kwamba yeye ni mkali ya stage Tanzania.
Kama ananizidi mimi, promota amlipe yeye ila
mimi kama H.Baba nitaperform bure na nitakuja
peke yangu na yeye inatakiwa aje peke yake. Kwa
sababu kuna Kiswahili fasaha ambacho
kinakosewa kuna neno linaitwa mtumbuizaji bora
na kuna watumbuizaji bora. Mimi ni mtumbuizaji
bora, wengine ni watumbuizaji bora. Kwanini
nasema watumbuizaji bora kwa sababu msanii
yeye mwenyewe hajiwezi mpaka awe na watu
wakucheza naye, ila mimi binafsi najiweza kwa
sababu mimi mwenyewe ninaweza fanya kazi na
ikaeleweka.
Ndiyo maana ya hii tuzo niliyopata leo.
Ninaowatambua walikuwa watumbuizaji na
ninawaheshimu mpaka leo nawataja watu wawili,
kuna Mr Nice kuna TID (Top In Dar ) hao ndo
watu wanaweza kusimama kwenye show na
kuburudisha na watu wakasema asante.” |
0 comments:
Post a Comment