Monday, September 15, 2014
 |
| HII sasa ni kufuru!” Hivi ndivyo
utakavyoweza kusema kwa Davies Mosha
ambaye ni makamu mwenyekiti wa zamani wa
klabu ya Yanga, ambaye nafasi yake kwa sasa
klabuni hapo inashikiliwa na Clement Sanga.
Kwa tafsiri ya haraka, yawezekana Mosha
anaweza kuwa ndiye kiongozi pekee wa soka
nchini kumiliki gari la kifahari na lenye
gharama kubwa aina ya Lamborghini kama
ambalo linamilikiwa na mshambuliaji
wa Manchester United, Wayne Rooney.
Gari analomiliki Mosha ambalo lina rangi ya
njano, linaaminika kuwa miongoni mwa
magari yenye thamani kubwa siyo tu Tanzania
na Afrika, bali duniani kote, kwani hata siku
Rooney alipolinunua wenzake wengi
hawakutegemea, siyo kwa sababu hana fedha,
ila kwa kuwa hakuwa mtu wa matumizi ya
magari yenye thamani kubwa kama hilo.
Mosha ameliambia Championi Ijumaa kuwa
anamiliki magari kadhaa ya kifahari kwa
matumizi yake binafsi na familia yake.
Yafuatayo ni maelezo kuhusiana na gari hilo la
kifahari kwa kuanzia kiwango cha mafuta na
usumbufu anaoupata akiwa katika mizunguko
yake.
Ameinunua kwa bei gani?
“Kutokana na ubora wa gari hili, nililazimika
kutoa shilingi bilioni moja kwa ajili ya
kulinunua, kama unavyojua ni fedha nyingi,
nimenunua kwa mapenzi yangu.
Mmiliki wa gari hili
Alipolinunua
“Hili gari kaniuzia mtoto wa Bakhresa
(Yusuph), baada ya kufikia makubaliano kati
yake na mimi, aliniuzia Julai 2011.
Spidi ya gari
“Hili gari kasi yake ya mwisho ni 360, ni kasi
kali na inatosha kwa matumizi yangu binafsi.
Matumizi ya mafuta
“Matumizi ni ya kawaida wala siyo ya
kuogopesha sana, inategemea na umbali
utakaotembea.
Usumbufu anaoupata
“Usumbufu mkubwa ninaoupata kiukweli,
nikiwa naendesha barabarani, madereva
wengine wanalishangaa sana, hali
inayosababisha kutokea ajali au msuguano
mara kadhaa.
“Hivi karibuni dereva mmoja aliigonga sehemu
ya tairi la nyuma kushoto kutokana na
kuishangaa, ilikuwa maeneo ya Masaki
hapahapa Dar es Salaam.
“Matengenezo yake yaligharimu pauni 20,000
(zaidi ya shilingi milioni 50), hali
iliyosababisha niwe makini nikiwa naendesha,”
anasema Mosha.
“Matengenezo yake yaligharimu pauni 20,000
(zaidi ya shilingi milioni 50), hali
iliyosababisha niwe makini nikiwa naendesha,”
anasema Mosha. |
 |
| Huyu ndo mmiliki wa gari hiyo |
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment