Tuesday, September 30, 2014

CHEKI KEANE NA BOSI WAKE WALIVYOMPOTEZEA JOSE MOURINHO

Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho haishi vituko, lakini safari hii alikutana na kali zaidi. Katika mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Aston Villa, wakati Chelsea inaongoza kwa mabao 3-0, zikiwa zimebaki dakika chache kabla ya mechi kwisha, akainuka na kwenda kwenye benchi ka Aston Villa na kutaka kuwapa mkono makocha. Kocha Mkuu, Paul Lambert kwanza akagoma na kuhoji muda ulikuwa bado, baadaye akatoa mkono kishikaji. Lakini msaidizi wake, Roy Keane wala hakuwa na habari, wakati Mourinho anampa mkono, yeye akaendelea kuangalia mechi. Mourinho akajitahidi kumgonga begani, Keane akaendelea kuuchupua na Mourinho akachukua zake time.

0 comments:

Post a Comment